Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:55

Aung San Suu Kyi alaumiwa kwa kupuuzia mauaji ya Waislam Myanmar


Aung San Suu Kyi
Aung San Suu Kyi

Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi amesimamisha mpango ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Matiafa (UN) mwezi huu baada ya kukabiliwa na lawama za kushindwa kulisimamia swala la machafuko huko Myanmar.

Machafuko hayo yamelazimisha Waislamu wa kabila la Rohingya takriban 370,000 kukimbilia kuvuka mpaka wa Bangladesh.

Msemaji wa serikali Zaw Htay amesema mapema leo kwamba mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel atabaki nchini Myanmar kushughulikia hali ya usalama iliyo-mashakani kwa sasa.

Aung San Suu Kyi, amekuwa taswira ya demokrasia kutokana na kushikiliwa kwake kwa kipindi kirefu na utawala wa zamani wa Myanmar wa kijeshi.

Lakini msimamo wake tofauti dhidi ya matatizo yanayowakabili Waislam wa Rohingyas katika jimbo la Rakhine- akikanusha kuwa habari nyingi juu ya tatizo hilo ni “taarifa za uongo” ambazo zinalengo la kusaidia maslahi ya “magaidi”.

Kauli yake hiyo imemsababishia kupoteza heshima yake kwa serikali mbalimbali na wanaharakati wa haki za kibinadamu ulimwenguni, wakiwemo baadhi ya wale waliowahi kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kama yake.

Vyanzo vya habari nchini Myanmar vinaeleza kuwa Waislam wa nchi hiyo wamekuwa wakikimbia kuelekea India na Bangladesh.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, helikopta za kijeshi zimeendelea kupiga risasi maeneo ya Waislam.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa kwa miaka 10 iliyopita, Jeshi la nchi hiyo limekuwa likiwatafuta watu wazima wa jamii hiyo ya Waislam na kuwaua na ndiyo sababu watu wa Rohingya wanakimbilia Bangladesh. Hata hivyo serikali ya Myanmar imekanusha tuhuma hizo dhidi ya Jeshi lake.

Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi zinazoshughulikia wakimbizi zikifanya kazi na Umoja wa Mataifa, kiasi cha Waislam wa Rohingya 400 waliuawa wakati wa machafuko hayo na wakati upelelezi ukifanywa na Jeshi.

Kufuatia mauaji hayo Takriban Waislam 40,000 wameondoka kutoka katika makazi yao huko Myanmar na sasa wanapata hifadhi katika majimbo ya Hyderabad, Jammu, Delhi, West Bengal, Uttar Pradesh, Punjab na Rajasthan nchini India.

XS
SM
MD
LG