Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:53

Wahindu wakimbia mauaji Myanmar


Wanawake wa Kihindu walioweza kukimbia vita huko Rakhine baada ya kuwasili Bangladesh Agosti 28, 2017.
Wanawake wa Kihindu walioweza kukimbia vita huko Rakhine baada ya kuwasili Bangladesh Agosti 28, 2017.

Wahindu ambao wamekimbia vita nchini Myanmar tangu Agosti na kuwa wakimbizi Bangladesh wakiwa pamoja na Waislam wa Rohingya, wanasema hawako tayari kurudi Myanmar.

Wanadai kuwa kuna uvunjifu wa amani katika vijiji vyao katika jimbo la Rakhine na hawako tayari kurudi huko kwa sababu wanawasiwasi wakukabiliwa na mauaji.

Wakimbizi wa kabila la Wahindu huko Bangladesh wamesema kuwa wanataka kuhamia India iwapo serikali ya Myanmar haitawasaidia kupata makazi mapya katika maeneo yaliyokuwa na Wabudha wengi katika nchi hiyo.

“Vijiji vyetu katika eneo la Rakhine haviko salama kabisa kwa Wahindu. Iwapo serikali ya Myanmar itatusaidia kuhamia Rangoon tuko tayari kuenda huko,” Lolimohan Sil, miaka 52, kinyozi kutoka eneo la Bolibazar, ameiambia VOA.

“Iwapo Myanmar haiwezi kutusaidia kwenda kukaa maeneo salama na yenye amani katika nchi hiyo tunataka kuhamia India, na India ni lazima itusaidie.”

Mwezi moja baada ya waasi wa Rohingya kushambulia vituo vya polisi 30 na kambi ya jeshi na kuuwa watu 12, iliyosababisha jeshi kufanya operesheni maalum dhidi ya vijiji vya Rohingya, serikali ya Myanmar imeripoti kupatikana miili 45 ya Wahindu katika makaburi ya pamoja matatu katika vijiji walikokuwa wanaishi.

Maafisa wa Myanmar wamesema kuwa ilikuwa ni wapiganaji wa Kiislam wa Rohingya waliofanya mauaji ya zaidi ya Wahindu 90, wakiwemo wale ambao miili yao ilipatikana katika makaburi ya pamoja.

Hata hivyo waasi wa kikundi cha Arakan Rohingya Salvation Army (ARSA) wamekanusha kuwaua Wahindu, na kuwa walikuwa hawajashambulia raia wowote.

Tangu Agosti 25, zaidi ya Waislam wa Rohingya 600,000 wamekimbia makazi yao na kuvuka mpaka wa Bangladesh. Pia Wahindu 800 wamekimbia kutoka Myanmar.

Mara baada ya kuwasili Bangladesh, wakimbizi Wakihindu waliwaambia waandishi wa habari wa Bangladesh wamesema kuwa ndugu zao wapenzi waliuwawa na vikosi vya usalama vya Myanmar na Wabudha wanaume wa eneo la Rakhine Myanmar.

Hivi sasa, hakuna mtu yoyote kutoka katika jamii hiyo ya wakimbizi wa Kihindu anayesema kuwa wanajeshi wa Myanmar au wakazi wa nchi hiyo walimuua Mhindu yeyote. Baadhi ya wakimbizi wa Kihindu wanasema hawakuweza kuwatambua wauaji kwa sababu walikuwa wameficha nyuso zoa.

Wengine wao wanasema kuwa waasi wa Rohingya waliwaua ndugu zao na majirani wa kihindu.

XS
SM
MD
LG