Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:53

Bunge la Marekani laandaa muswada dhidi ya jeshi la Myanmar


Waislam wa Rohingya waliovuka mpaka kutoka Myanmar kuingia Bangladesh, wakiwa katika eneo la shule katika kambi ya wakimbizi ya Kutupalong rest inside a school compound at Kutupalong Oct. 23, 2017.
Waislam wa Rohingya waliovuka mpaka kutoka Myanmar kuingia Bangladesh, wakiwa katika eneo la shule katika kambi ya wakimbizi ya Kutupalong rest inside a school compound at Kutupalong Oct. 23, 2017.

Hata kabla ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kufikia ukweli iwapo mauaji ya jeshi la Myanmar dhidi ya Waislam wa Kabila la Rohingya kuwa ni mauaji ya kikabila, wawakilishi wa Bunge la Congress wanaweka shinikizo juu ya serikali ya nchi hiyo kukabiliana na mgogoro huo.

Maazimio yaliyofikiwa na bunge hilo na Baraza la Seneti ikiwa ni pamoja na kulaani uvunjifu wa amani na kutoa agizo kwa kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi kutoa tamko la nguvu juu ya suala hilo.

Kutoa shinikizo hilo ni mwanzo wa Bunge la Marekani kuchukua hatua ambayo hatimaye itapelekea kuwepo muswada unaojitosheleza kuelekea kwenye vikwazo dhidi jeshi la Myanmar.

Lakini wabunge kama vile Seneta Richard Durbin Mdemkorati amesema Myanmar, ambayo inajulikana kama Burma, ni lazima ichukue hatua hivi sasa.

“Hatutaki kusubiri kupitishwa kwa azimio hili, hata kama itakuwa ni ishara yakuonyesha umuhimu wake. Tunataka kuona matokeo,” Durbin ameiambia VOA.

“Tunatoa wito kwa serikali hii, tunamuagiza Aung San Suu Kyi, kuingilia kati suala hili, apaze sauti na kuchukua hatua.”

Seneta Durbin na baadhi ya wabunge wa Warepublikan na Wademokrati walikutana na balozi wa Myanmar wiki hii na kumuambia uhusiano wa nchi yake na Marekani unategemea jinsi watavyoweza kukabiliana na mgogoro huu.

Durbin amesema wabunge hao wanataka vyombo vya dola viruhusu wachunguzi wa nje wafike katika maeneo yenye vita, kuwafanya askari waliohusika na mauaji kuwajibika.

Pia vyombo hivyo vifanye kazi na wakala wanaosimamia wakimbizi wa Umoja wa Mataifa ili kuweza kuwatafutia makazi wale waliosambaratishwa na vita hivyo.

“Iwapo watakuwa hawako tayari kuruhusu wachunguzi wa nje kuingia katika eneo hilo ambako maagamizi yaliyopita kifani yametokea, ambapo madhila makubwa yanawakabili watu wa Rohingya, ni lipi litatufanya katika ulimwengu wa leo kutoa fungu la kwanza la Dola za Marekani kuipa nchi ya Myanmar?” ameuliza Durbin.

Mpaka sasa hivi haifahamiki kwa kiasi gani Wabunge wa Marekani wanaafikiana na hatua kali zinazotakiwa kuchukuliwa na Marekani dhidi ya Myanmar.

XS
SM
MD
LG