Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 07:01

UN yatathmini hali ya wakimbizi 700,000 walioko Bangladesh


Rais wa Baraza la Usalama Gustavo Meza-Cuadra (wa pili kushoto) akiwa na timu ya Baraza la Usalama la UN wakati walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa Naypyitaw, Myanmar, April 30, 2018.

Wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza uvunjifu wa haki za binadamu nchini Myanmar wamekutana na kiongozi anayetambulika nchini humo, Aung San Suu Kyi, walipotembelea Bangladesh, ambako wakimbizi 700,000 wamekimbilia kufuatia machafuko katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar.

Ujumbe wa watu 15 wa Baraza la Usalama la UN wamekutana Jumatatu na Aung San Suu Kyi, na kamanda mwandamizi wa jeshi Jenerali Min Aung Hlaing huko Naypyitaw.

Ujumbe huo wa UN utaelekea kwenye jimbo la Rakhine lenye machafuko Jumanne kuangalia athari za ukandamizaji uliofanywa na jeshi ulioanza Agosti 2017, pamoja na matayarisho ya kurejeshwa kwa wakimbizi, wengi wao ni wa kabila la Rohingya walio wachache.

Warohingya wamekataliwa uraia, pamoja na kuwa wengi katika familia hizo wameishi katika nchi ya Myanmar kwa vizazi vingi. Wakimbizi wamekimbia uvunjifu wa amani katika jimbo la Rakhine ambao UN imeeleza kuwa unalingana na nadharia halisi ya mauaji ya kikabila”.

Serikali ya Myanmar imekubali kuruhusu wajumbe wa UN kutembelea eneo la Rakhine, baada ya siku za nyuma kukataa kamati ya uchunguzi kuingia eneo hilo. Waandishi wa habari na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wamezuiliwa kuingia katika jimbo hilo kwa miezi kadhaa sasa.

Ujumbe wa UN uliwasili Jumamosi nchini Bangladesh ili kuweza kujioneya wenyewe hali ya wakimbizi wa Rohingya, kutembelea eneo la Cox Bazar ambapo kambi za wakimbizi za muda zimefunguliwa mpakani karibu na Myanmar.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG