Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 16:20

Mjukuu wa Nelson Mandela afariki dunia


Mjukuu wa Nelson Mandela, Zoleka (kushoto) akiwa na Ndileka Mandela walipowasili katika hospitali ya MediClinic Heart huko Pretoria ambako rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alikokuwa amelazwa Julai 1, 2013. Picha na ERIC FFEFERBERG / AFP.
Mjukuu wa Nelson Mandela, Zoleka (kushoto) akiwa na Ndileka Mandela walipowasili katika hospitali ya MediClinic Heart huko Pretoria ambako rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alikokuwa amelazwa Julai 1, 2013. Picha na ERIC FFEFERBERG / AFP.

Mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Nelson Mandela, Zoleka Mandela, amefariki dunia kwa saratani akiwa na umri wa miaka 43, familia yake ilisema Jumanne.

Alikuwa akijulikana kwa kuelezea vita vyake vya muda mrefu dhidi ya ugonjwa huo, mwandishi huyo wa vitabu, alilazwa hospitali siku ya Jumatatu kama sehemu ya matibabu yake aliyokuwa akiendelea nayo, msemaji wa familia alisema.

"Zoleka alifariki... akiwa amezungukwa na marafiki na familia," alisema Zwelabo Mandela.

Zoleka alikuwa mtoto wa binti wa mwisho wa Mandela, Zindzi Mandela, na mume wake wa kwanza, Zwelibanzi Hlongwane.

Familia hiyo ilisema uchunguzi wa hivi karibuni ulionyesha kusambaa "kwa kiasi kikubwa" kwa saratani ambayo iliathiri nyonga, ini, mapafu, ubongo na uti wa mgongo.

"Tunaomboleza kumpoteza mjukuu mpendwa wa mama Winnie na Madiba," Wakfu wa Nelson Mandela uliandika kwenye mitandao ya kijamii, ukitumia jina maarufu la mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG