Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:54

Zambia na China zaahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alipodhuria mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. Picha na Reuters
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alipodhuria mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. Picha na Reuters

Rais Xi Jinping alisema siku ya Ijumaa kuwa China inaiunga mkono Zambia katika kulinda uhuru wa taifa lake, usalama na maslahi ya maendeleo, wakati akishawishi uagizaji zaidi wa bidhaa kutoka nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Xi alikutana na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema mjini Beijing kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa "ushirikiano wa kina na wa kimkakati," shirika la habari la serikali ya China Xinhua alisema.

Rais Xi alisema mwezi Julai kuwa kuendeleza ushirikiano na nchi za kiafrika “ ni hatua muhimu katika msingi” wa sera za mambo ya nje ya China.

Zambia inatafuta kurekebisha deni lake la nje na

China na kupata fursa zaidi za biashara na nchi hiyo yenye

uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.

China na Zambia zilitoa taarifa ya pamoja Ijumaa jioni, bila kutaja makubaliano yoyote kuhusiana na madeni.

Hata hivyo, nchi zote mbili zitashinikiza matumizi makubwa ya Sarafu za ndani katika biashara na uwekezaji wao, Shirika la habari la China la Xinhua liliinukuu taarifa hiyo ya pamoja ikisema.

China ina maslahi makubwa ya kibiashara nchini Zambia, ikiwa imewekeza katika miradi zaidi ya 30 kupitia mpango maarufuku unaojulikana ka Belt and Road Initiative kati ya mwaka 2014 na 2023, kulingana na data ziliyokusanywa na Taasisi ya American Enterprise.

Inaonyesha miradi hiyo ilikuwa na thamani ya jumla ya dola bilioni 11.3, kuanzia sekta ya nishati hadi kilimo na usafiri wa anga. China pia inachukua takriban moja ya tano ya mauzo ya nje ya Zambia, hususani shaba.

Rais Xi alisema China inashawishi uingizaji zaidi wa bidhaa zenye ubora wa juu kutoka Zambia kuingia katika soko la China na kuyasaidia makampuni zaidi yanayofadhiliwa na China yanayowekeza nchini Zambia.

Rais Hichilema atakuwa nchini China hadi Jumamosi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG