Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 05:07

G-20 kuipa Afrika Sauti katika uchumi wa dunia


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi (katikati), Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na viongozi wengine wakati wa mkutano wa G20 huko New Delhi, Septemba 10, 2023. Picha na PIB / AFP.

Umoja wa Afrika kuniga katika kundi la G20, lenye nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani kunaangazia ushawishi unaokua wa bara hilo na kuwapa viongozi wake sauti yenye nguvu zaidi katika kufanya maamuzi duniani.

Viongozi wa Afrika wameipongeza hatua hiyo kwa uwakilishi mzuri wa Ulimwengu wa Kusini na kuitambua Afrika katika mijadala ya kimataifa kuhusu matatizo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa ambapo mara nyingi yamekuwa yakiliathiri zaidi bara hilo, lakini ni mara chache sana hushauriwa.

Wakati China na Russia zikisisitiza ushawishi zaidi, na kundi la biashara la BRICS likiwa limepanuka na kujumuisha nchi za Misri na Ethiopia, wachambuzi na wataalamu walisema uamuzi wa G20 pia unaonyesha uzito wa Afrika kama mdau wa kipekee wa kimataifa.

Umoja wa Afrika wenye nchi wanachama 55 unaojiunga na G20, kundi hilo limelijumisha bara linalokuwa kwa kasi zaidi na lenye idadi kubwa ya vijana na uwezo mkubwa wa kuchangia katika kuendeleza mabadiliko ya kijani.

Shinikizo la wanachama wa G20 liliongezeka mwaka huu, huku rais wa Senegal Macky Sall akisema kiti cha AU kitaondoa "ukosefu wa haki" na mkuu wa benki kuu ya EU Christine Lagarde akisihi uwepo wa uzito zaidi kwa Afrika katika taasisi za kifedha.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi alitangaza kujiunga kwa AU katika kundi la G20 wakati wa mkutano wa kilele uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini New Dehli.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, akimkumbatia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na pia rais wa Comoro Azali Assoumani wakati wa mkutano wa G20 Septemba 9, 2023. Picha na Evan Vucci/ REUTERS.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, akimkumbatia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na pia rais wa Comoro Azali Assoumani wakati wa mkutano wa G20 Septemba 9, 2023. Picha na Evan Vucci/ REUTERS.

"Uanachama wa kudumu wa Afrika katika G20 unamaanisha kuwa imetambuliwa kama mhusika mkuu katika nyanja ya uchumi wa dunia," Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alisema kupitia mtandao wa X, uliokuwa ukijulikana kamaTwitter.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ambaye anataka kuiweka nchi yake, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika na taifa lenye watu wengi, kurudi kwenye ramani kama nchi yenye uzito mkubwa wa kikanda, ameipokea hatua hiyo inayoelekea katika ujumuishaji mkubwa.

Tinubu, ambaye anaongoza jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi ECOWAS, alisema pia Nigeria inatazamia kuchukua jukumu kubwa.

"Nigeria imejiandaa, ina uwezo na iko tayari kuwa mshiriki mkuu katika familia hii ya G20 na katika kuunda ulimwengu mpya, ambao bila wao, familia itabaki kuwa haijakamilika," alisema rais Tinubu katika taarifa yake.

Wachambuzi walisema wakati AU tayari ina fomula ya kuwa na kauli ya pamoja miongoni mwa wanachama wake 55, itahitaji kuongezea muundo ili kufanikisha masuala ya G20.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG