Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:08

Biden anaelekea katika mkutano wa viongozi wa G20, Xi na Putin hawatarajiwi kuhudhuria


Mchoraji wa India Jagjot Singh Rubal akimalizia kwa rangi ya mafuta mchoro wa Rais wa Marekani Joe Biden, katika ofisi yake huko Amritsar Septemba 5, 2023, kabla ya kuanza kwa mkutano wa siku mbili wa G20, New Delhi. (Picha na Narinder NANU / AFP)

White House ilisema hayo Jumanne, huku kukiwa na uvumi kuhusu afya ya Rais Biden baada ya mkewe Jill Biden kugundulika ana maambukizi ya COVID-19 siku moja kabla.

“Hana ishara zozote za maambukizi,” msemaji wa White House Karine Jean-Pierre alisema, akiongeza kuwa Biden alipima Jumanne asubuhi na hana maambukizi na atapimwa katika utaratibu utakaoamuliwa na daktari wake.

Hakusema kitu, alipoulizwa, utaratibu gani utafuatwa iwapo atagundulika ana maambukizi kabla ya safari yake ya Alhamisi kuelekea New Delhi.

Mshauri wa usalama wa taifa Jake Sullivan alisema uongozi utajikita katika masuala kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, kurekebisha muundo wa madeni na vita vya Ukraine. Mkusanyiko huo unaanza siku ya Jumamosi katika mji mkuu wa India.

Jake Sullivan
Jake Sullivan

Wachambuzi wanasema kutokuwepo kwa viongozi wakuu wawili – Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping – kutaathiri mazungumzo ya mkutano, hususan juu ya changamoto kubwa inayomkabili mwenyeji wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

“Kituko kikubwa katika mkutano huu wa mjini New Delhi ni iwapo nchi hizo zitaweza kufikia makubaliano ya pamoja, ambayo walifikia mwaka jana katika mkutano wa mwisho huko Bali, tamko lililokuwa na ibara kadhaa ambazo Russia ilikubali, kama taarifa hiyo ilivyojieleza, kuwa ilikuwa imefanya uchokozi nchini Ukraine,” alisema profesa John Kirton, ambaye anaongoza Kikundi cha Utafiti katika Chuo Kikuu cha Toronto. Alizungumza na VOA kupitia mtandao wa Zoom.

“Iwapo Bw Modi ataweza kuitisha makubaliano ya kimaandishi kama vile alivyofanya Rais Joko Widodo wa Indonesia mwaka jana, itabidi tusubiri tujionee.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Lakini nafikiri ni habari njema kuwa Putin tena ameamua kutohudhuria mkutano huo, kama alivyofanya ulipofanyika Bali mwaka jana. Inaelekea kama Xi Jinping wa China hatahudhuria. Hiyo itarahisisha kuzifanya nchi zote nyingine kuchukua hatua.”

Biden alisema hivi karibuni kuwa alisikitishwa kuwa kiongozi imara wa China alikuwa hajapanga kuhudhuria.

Hata hivyo, alisema, “Nitafanya utaratibu wa kuonana naye.”

Sullivan, Jumanne, hakusema wakati gani mkutano huo unaweza kufanyika.

Wachambuzi wanasema wanatarajia kuwa New Delhi na Beijing wanaweza kuweka kando tofauti zao juu ya ramani mpya ya China ambayo India inaikataa.

Forum

XS
SM
MD
LG