Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 20:09

Biden aelekea India kwa mkutano wa G20


Biden akipanda ndege kwelekea kwa mkutano wa G20 nchini India

Rais wa Marekani Joe Biden aliondoka mjini Washington Dc Alhamisi kuelekea kwa mkutano wa kilele wa G20 nchini India, akitumai kutumia nafasi ya kutokuwepo kwa viongozi wa China na Russia ili kuimarisha ushawishi wa Marekani katika umoja huo uliogawanyika, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Biden atajaribu kuonyesha kwamba katika masuala makubwa ya kimataifa, Washington ni mshirika bora kuliko Beijing au Moscow, na kwamba G20 inasalia kuwa jukwaa muhimu, AFP iliripoti Alhamisi.

Lakini mgawanyiko mkubwa kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine na jinsi ya kusaidia mataifa yanayoibukia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, unatarajiwa kutatiza makubaliano wakati wa mkutano wa siku mbili mjini New Delhi.

Biden pia atazuru Vietnam siku ya Jumapili ambapo anatarajiwa kuimarisha uhusiano na hasimu huyo wa zamani wa Marekani, katika jitihada zaidi za kukabiliana na ushawishi wa China unaoongezeka.

Ndege ya rais, Air Force One, iliondoka Joint Base Andrews karibu na Washington na inatarajiwa kuwasili India siku ya Ijumaa.

Forum

XS
SM
MD
LG