Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 01:29

Afrika ya kusini yaonya uhaba wa kuku na mayai



Kuku wakiwa kwenye shamba la kuku huko Hartbeesfontein Afrika Kusini, Agosti 15, 2018. Picha na REUTERS/Siphiwe Sibeko
Kuku wakiwa kwenye shamba la kuku huko Hartbeesfontein Afrika Kusini, Agosti 15, 2018. Picha na REUTERS/Siphiwe Sibeko

Wafugaji kuku nchini Afrika Kusini wameonya kuhusu uwezekano wa uhaba wa kuku na mayai huku wakipambana na kile ambacho sekta hiyo inasema ni mlipuko mbaya sana wa mafua ya ndege ambao haujawahi kutokea nchini humo.

Afrika Kusini ni moja ya wazalishaji wakubwa wa kuku barani Afrika, imeripoti visa vya kwanza vya mafua ya ndege katika mashamba ya biashara mwezi Aprili, kulingana na kundi la viwanda.

Kampuni ya uzalishaji ya Quantum Foods imesema Ijumaa kuwa mwaka huu kampuni hiyo imepoteza takriban kuku milioni mbili -- wenye thamani ya jumla ya zaidi ya dola milioni 5.3 kutokana na ugonjwa huo.

"Afrika Kusini inashuhudia mlipuko mbaya sana wa mafua ya ndege," kampuni nyingine mzalishaji wa kuku ya Astral alisema katika maelezo yake ya biashara siku ya Alhamisi.

Mlipuko huo mpaka sasa umeigharimu kampuni hiyo randi milioni 220 hadi sasa, ilisema kampuni.

Mafua ya ndege kwa kawaida haiambukizi binaadamu. Lakini H5N1 imekuwa ikizidi kuwaambukiza mamalia duniani kote, kuanzia simba wa baharini nchini Argentina hadi mbweha nchini Finland na hivyo kuzua hofu kuwa inaweza kuambukizwa kwa wanadamu kwa urahisi sana.

Kwa kawaida virusi vimekuwa vikizuka kwa msimu, lakini tangu mwaka 2021 kesi zimekuwa zikiibuka mwaka mzima, na duniani kote, na kusababisha kile ambacho wataalam wanasema ndio mlipuko mkubwa zaidi ambao haujawahi kuonekana.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG