Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 22:41

Mkutano wa AGOA utafanyika Afrika Kusini licha ya upinzani, Marekani yasema


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Kushoto) na rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Kushoto) na rais wa Marekani Joe Biden.

Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa biashara kati ya Marekani na Afrika mwezi Novemba licha ya wito wa awali wa wabunge wa Marekani kutaka hafla hiyo ihamishwe kutokana na  kile walichosema ni kuimarika kwa uhusiano wa kijeshi kati ya nchi hiyo na Russia.

Kitovu cha uchumi cha Afrika Kusini, Johannesburg, kitakuwa mwenyeji wa Kongamano la Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi la Marekani na Kusini mwa Jangwa la Sahara, kuanzia Novemba 2 hadi 4, maafisa wa Marekani na Afrika Kusini walisema katika taarifa ya pamoja siku ya Jumatano.

Mkutano huo utajadili mustakabali wa mpango wa Ukuaji na Fursa kwa Afrika, maarufu kama AGOA, programu kuu ya biashara ya Washington kwa bara hilo, ambayo inaruhusu bidhaa kuingia kwa soko la Marekani bila kutozwa ushuru, na ambao unatazamiwa kufika mwisho Septemba 30, 2025.

"Kama Rais Biden alivyosema, Afrika ndio mstakabal wa dunia," Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Katherine Tai alisema katika taarifa hiyo. Tai alisema alitarajia kuzuru Afrika Kusini "kujadili fursa za kuifanyia AGOA mabadiliko."

Kufuatia uvamizi wa Russia nchini Ukraine, maafisa wa Marekani na Ulaya wamejaribu kupinga hatua za Moscow miongoni mwa serikali za Afrika. Mataifa mengi ya Afrika, hata hivyo, yamekataa kuegemea upande wowote.

Forum

XS
SM
MD
LG