Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 21:12

Mawaziri wa nchi wanachama wa COMESA wataka bajeti za miundombinu ziongezwe


Wajumbe waliohudhuria mkutano mwa mawaziri wa nchi wanachama wa Comesa mjini Kigali, Rwanda. Picha na Sylvanus Karemera/ VOA.

Mawaziri wa Nchi za jumuiya ya kiuchumi ya mashariki na kusini mwa Afrika Comesa, wanaokutana mjini Kigali, Rwanda, wamesema kwamba kuna haja ya kuongeza maradufu bajeti zinazoelekezwa kwa miundombinu katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Wakizungumza katika mkutano uliofanyika Alhamisi mjini Kigali, Rwanda, mawaziri wanaohusika na miundombinu wamesema kwamba nchi nyingi zina nia ya kuungana kiuchumi lakini tatizo la miundo-mbinu isiyotosha limekuwa ni changamoto kubwa.

Jumuiya hiyo inaundwa na mataifa 21 yenye lengo la kurahisisha uhusiano wa kibiashara,miundo mbinu pamoja na raslimali ili kuinua kiwango cha maendeleo ya kiuchumi miongoni mwa nchi hizo.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:42 0:00

Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari wa Burundi Bi Leocadia Ndacayisaba amesema amesisitiza ushirikiano huo ikiwa nchi za Comesa zinataka kuharakisha kupata maendeleo endelevu.

"Ni muhimu sana kwa mataifa wanachama kuweka juhudi zao pamoja ili kutafuta suluhisho la changamoto za miundo ambazo hadi sasa zinaendelea kudhoofsha maendeleo yetu. Kwa pamoja tunaweza kushirikiana na kurahisisha kasi ya maendeleo yetu ambayo hadi sasa ni kama yamekwama," alisema.

Moja ya changamoto ambazo hadi sasa zimekuwa mzizi wa majadiliana haya ni pamoja na tatizo la ukosefu wa mawasiliano rahisi miongoni mwa waafrika wenyewe kutokana na sheria kali au miundombinu isiyotosha au isiyokuwepo kabisa.Huyu ni Patricia Uwase ambaye ni naibu waziri katika wizara ya miundombinu ya Rwanda

"Bado tunaona kwamba ni kama haiwezikani kusafiri kwa ndege barani afrika,kwa hiyo mkutano huu ni jukwaa la pamoja la mawaziri wa miundo mbinu pamoja na watunge sera wengine kuweza kurejea kule na kutafuta sababu inayosababisha hali hii kuwepo," alisema.

Mkurugenzi mkuu katika wizara ya nishati ya Kenya Mhandisi Benson Mwakina ameyataja baadhi ya matarajio ya mkutano huu

Yeye pia licha ya kuwa na imani kwamba mkutano huu utachukua maazimio bado ana wasiwasi

Katika mazungumzo yanayoendelea pia kuna hili la uwezekano wa siku zijazo nchi za jumuiya ya Comesa zikaoanisha leseni za magari ili kuondoa vizuizi vya sasa vinavyozuia maendeleo ya nchi hizi.

-Imetayarishwa na Sylivanus Karemera, Kigali, Rwanda

Forum

XS
SM
MD
LG