Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 13:47

Mgombea nafasi ya Jumuiya ya Madola anadi ajenda yake, Jamaica yataka mabadiliko


Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamaica Kamina Johnson Smith.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamaica Kamina Johnson Smith.

Nchi yake wakati huohuo ilitoa taarifa kutetea ugombea wake baada ya katibu aliyeko madarakani hivi sasa kumtaka kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.

Katika taarifa ya Mei 12, serikali ya Jamaica ilisema uteuzi wake uliwasilishwa “katika dhana ya mwelekeo wa mabadiliko ya uongozi ambayo yalionekana ni dhahiri na nchi wanachama katika kila upande.

Kwa kweli, kadri muda unavyokwenda, nchi mbili wanachama [Kenya na Tuvalu] zilitangaza wagombea wake kwa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu, wakionyesha dalili ya kutaka mabadiliko kwa bara la [Afrika na Pacific].

Mgombea wa Kenya hivi karibuni alijiondoa, na ikionyesha matumaini kuwa mgombea mwengine atajitokeza.”

Jamaica imesema ilikuwa na wajibu wa kufafanua msimamo wake kwani “katika mchakato mpana wa kuwasiliana baina ya nchi za Jumuiya ya Madola, nchi kadhaa zimekuwa zinauliza kuhusu uwepo wa wagombea wawili kutoka nchi wanachama wa Caribbean, na pia maelezo mapya kuhusu ‘kutokuwepo nafasi’ katika ofisi hiyo.”

Wito wa kujiondoa katika kinyang'anyiro

Katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha televisheni cha ABSTV, katibu mkuu aliyeko madarakani Patricia Scotland alipendekeza kuwa Bi Johnson-Smith ajiondoe katika kinyang’anyiro hicho.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland,
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland,

Nitakuwa na furaha kubwa kama Seneta Kamina Johnson-Smith angefikiria tena na angehisi pengine huu siyo wakati muafaka kushindana… kwa nafasi hii.

Nimetumikia miaka sita ya kipindi cahngu cha miaka 8. Afrika wanatarajia kuwa watapata fursa kumpendekeza katibu mkuu wa Kiafrika mwaka 2024 nitakapomaliza kipindi changu cha pili,” Bi Scotland alisema.

Katika ziara yake, Bi Smith alikutana na wakuu wa nchi na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, na pia Rwanda na Msumbiji.

Mjini Nairobi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Kenya Macharia Kamau alisema nchi yake inakubaliana na Bi Smith kuona mabadiliko yanafanyika katika Jumuiya ya Madola.

Raia huyo wa Jamaica, ambaye ndiye aliyejitokeza hivi karibuni, ni mshindani pekee wa Scotland ambaye kipindi chake cha kwanza kilitakiwa kumalizika mwaka 2020.

Hatahivyo, nchi 54 wanachama zilikubaliana aendelee na wadhifa huo kutokana na janga la COVID-19.

Johnson-Smith na Scotland watawakabili wanachama wapiga kura wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola huko Kigali mwezi ujao.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African, Nairobi, Kenya

XS
SM
MD
LG