Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:26

Ramaphosa akatisha kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola


Rais Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amelazimika kurejea nyumbani kukabiliana na hali ya vurugu na hivyo kulazimika kukatisha kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika London, Uingereza.

Polisi walirusha risasi za mpira Ijumaa kusambaratisha umati mkubwa wa waandamanaji kabla ya kuwasili kwa Rais katika jimbo la Kaskazini Magharibi ambako vurugu zimetokea.

Mapambano makali yametokea katika eneo hilo ambapo waandamanaji wanadai ajira, makazi na kutokomezwa ufisadi.

Maduka yamevunjwa na kuibiwa, barabara zimewekwa vizuizi na magari yamechomwa moto.

Rais Ramaphosa ametoa wito kuwepo utulivu na ameamrisha polisi kujizuilia.

Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vimeripoti kuwa maafisa wa polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji ambao walikuwa wamechoma moto basi, kupiga mawe magari na kuziba barabara kwa kutumia matairi yanayowaka moto.

XS
SM
MD
LG