Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:47

Muandaaji wa mashindano ya urembo nchini Rwanda akamatwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono


Ramani ya Rwanda
Ramani ya Rwanda

Muandaaji wa mashindano ya urembo nchini Rwanda na mwanamuziki mashuhuri wa zamani amekamatwa Jumanne kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono, polisi wamesema.

Dieudonne Ishimwe kwa jina la umaarufu Prince Kid, alitiwa mbaroni kwa tuhuma za “uhalifu unaohusiana na unyanyasaji wa kingono, idara ya upelelezi ya Rwanda ( RIB) imesema.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 36 anakabiliwa na mashtaka ikidaiwa kwamba alitenda makosa dhidi ya washindani wa zamani wa Miss Rwanda kwa nyakati tofauti, msemaji wa RIB Thierry Murangira, ameiambia AFP.

Kesi hiyo itafikishwa kwa mwendesha mashtaka kwa muda unaofaa kulingana na sheria, Murangira ameongeza.

Ishimwe ni mkuu wa kampuni iitwayo Rwanda Inspiration Back up, ambayo huandaa mashindano ya urembo ya kila mwaka ya Miss Rwanda.

XS
SM
MD
LG