Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:37

Sweden yamrudisha mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda


FILE - Rais wa Rwanda Paul Kagame
FILE - Rais wa Rwanda Paul Kagame

Manusura wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Tutsi walikaribisha ishara yenye nguvu kutoka kwa maafisa wa Sweden na kuendelea kukata rufaa kwamba nchi nyingine zinazowahifadhi wahalifu kama hao waache kuidhinisha kutoadhibiwa.

Mamlaka ya Sweden imemrejesha mwanaume huyo raia wa Rwanda mjini Kigali anayetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Upande wa mashtaka wa Rwanda ulisema ulimpokea Jean Paul Micomyiza Jumatano na kuipongeza Sweden kwa mchango wake wa kupambana na kuepuka adhabu.

Micomyiza alikamatwa Sweden Novemba mwaka 2020 kwa kibali ya Rwanda .

Alishindwa katika rufaa dhidi ya kurejeshwa nchini humo Disemba mwaka 2021.

Aliishi Sweden kwa zaidi ya muongo mmoja. Anashutumiwa kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari kwa mchango wake wa kuwatafuta na kuwatambua Watutsi kwa ajili ya kuuwawa kwenye mauaji hayo wakati huo alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha taifa kilichopo Butare kusini mwa Rwanda.

XS
SM
MD
LG