Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Uingereza yafikia makubaliano na Rwanda kuwasaidia wanaotafuta hifadhi


 Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mkutano wa uwekezaji baina ya Uingereza na Afrika | London, Januari 20, 2020.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mkutano wa uwekezaji baina ya Uingereza na Afrika | London, Januari 20, 2020.

Uingereza imeingia makubaliano na Rwanda kuwahamisha baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi kwenda katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Serikali ya Rwanda itapokea malipo ya awali ya dola milioni 150 kushiriki katika mpango huo.

Waziri Mkuu Boris Johnson amekuwa akitoa maelezo ya mpango huo ambao utawafanya wanaume wasio na wake wanaoomba hadhi ya ukimbizi kupelekwa umbali wa kilomita 6,000 ili kupata makazi mapya nchini Rwanda.

Anasema anachukua hatua kuwazuia watu wanaofanya magendo. Serikali ya Uingereza iko katika shinikizo kuzuia maelfu ya watu kufanya safari hatari kuelekea kusini mwa Uingereza kwa kutumia boti ndogo.

Mashirika ya kutoa misaada yamelaani mpango huo wa kuwahamisha watu kama ukatili na kuelezea wasiwasi wao kuhusu rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Rwanda.

XS
SM
MD
LG