Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:38

Ramani pana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yazinduliwa na marais 3


Marais watatu wa Afrika Mashariki, (kutoka kulia) Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda and Paul Kagame wa Rwanda, walipokutana Entebbe, mji mkuu wa Kampala, June 25, 2013. (Picha na Reuters).
Marais watatu wa Afrika Mashariki, (kutoka kulia) Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda and Paul Kagame wa Rwanda, walipokutana Entebbe, mji mkuu wa Kampala, June 25, 2013. (Picha na Reuters).

Marais Uhuru Kenyata wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, na Paul Kagame wa Rwanda Ijumaa wamezindua ramani iliyopanuliwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia kuingizwa kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuwa mwanachama mpya katika jumuiya hiyo.

Rais wa DRC Felix Tchisekedi alitia saini mkataba wa kujiunga, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Nairobi iliyoandaliwa na Rais Kenyatta mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za EAC.

Rais Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa EAC alisema kujiunga kwa DRC kama mwanachama wa EAC kutaimarisha uchumi wa kikanda na ushindani barani huko na kote duniani.

Wakuu hao wa nchi wamesema kwamba katika siku za usoni, mawaziri na wataalamu wa kiufundi watafanya kazi kwa kasi kuhakikisha DRC inaunganishwa kwenye vyombo vya EAC ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Haki ya Afrika, Bunge la Afrika Mashariki na kamati za kisekta kuhusu masuala muhimu kama vile biashara , afya , usalama , fedha , elimu , miundo mbinu na ushirikiano wa kimataifa.

Wameongeza kusema kuwa kuingia kwa DRC katika EAC kutapanua biashara na ushirikiano wa kieneo.

XS
SM
MD
LG