Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 12:37

Marekani : Tanzania, Sudan kuondolewa katika viza ya bahati nasibu


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Serikali ya Marekani inatarajia kutangaza katazo pana zaidi la viza za kuingia nchini humo, afisa wa serikali ya Marekani amesema, hatua ambayo itawaathiri maelfu ya wahamiaji na kuanzisha upya mjadala iwapo sera hiyo inawabagua Waislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, Marekani itasitisha kutoa viza ambazo zinaweza kupelekea mtu kupata ukazi wa kudumu Marekani kwa raia wa Eriteria, Kyrgyzstan, Myanmar na Nigeria, kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Chad Wolf, amesema wakati akiongea na waandishi wa habari Ijumaa.

Serikali ya Marekani pia itaacha kutoa “visa zinazotolewa kwa mataifa tofauti” kwa wananchi wa Sudan na Tanzania, Wolf amesema.

Visa hizo – ambazo Trump amezikosoa siku za nyuma – zinapatikana kwa bahati nasibu kwa waombaji kutoka nchi zenye idadi ndogo ya wahamiaji walioko Marekani.

Viza za uhamiaji zinazokusudiwa kusitishwa ni tofauti na zile zisizo kuwa za uhamiaji ambazo zinatolewa kwa wanaofanya ziara Marekani, ambazo hazitoathiriwa na katazo hili, Wolf amesema.

Wolf amesema nchi hizo sita zimeshindwa kukidhi viwango vya kubadilishana taarifa na masuala ya kiuslama, iliyopelekea umuhimu wa katazo hili jipya.

Matatizo yaliyoelezwa na Wolf ni kati ya teknolojia inayotumika ya pasipoti za kusafiria na kushindwa kwa nchi hizo kubadilishana taarifa juu ya washukiwa wa ugaidi na wahalifu.

Katazo la awali la kusafiri – lililotolewa wakati Trump yuko katika wiki yake ya kwanza madarakani Januari 2017 – lilikuwa ni katazo lililohusisha takriban wahamiaji wote na wasafiri kutoka nchi saba zenye Waislamu waliowengi. Sera hiyo ilirekebishwa wakati mahakama ikiipinga, lakini Mahakama ya Juu ya Marekani hatimaye iliwafiki na kuipitisha Juni 2018.

Katazo hilo lilioko linahusisha nchi zenye Waislamu waliowengi ambazo ni Iran, Libya Somalia, Syria and Yemen. North Korea na Venezuela ambazo zinakabiliwa na katazo la viza, lakini hatua hizo huwaathiri wasafiri wachache ukilinganisha na wale wanaoruhusiwa kuingia Marekani.

XS
SM
MD
LG