Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 17:47

Wademokrat wamtaka Trump asitishe amri ya kiutendaji kuhusu uhamiaji


Kiongozi wa walio wachache katika Bunge la Marekani, Nancy Pelosi.
Kiongozi wa walio wachache katika Bunge la Marekani, Nancy Pelosi.

Takriban wiki moja baada ya Rais Donald Trump kusaini amri ya kiutendaji iliyokataza kwa muda wahamiaji kutoka nchi zenye waislamu wengi kuingia Marekani, wademokrat wamemsihi rais asitishe amri hiyo .

Mwandishi wa VOA ameripoti kuwa kuanzia maadamano yanayopinga sera hiyo mpaka mikusanyiko katika Mahakama Kuu iliyokuwa imekerwa, juhudi kubwa inafanyika kumaliza kizuizi hiki cha kusafiri katika bunge la Marekani.

Rais aenda kinyume cha Katiba

Wademokrat waliokasirishwa na hili wamemaliza wiki hii wakidai kwamba rais mpya tayari amevunja misingi aliyoapa kuisimamia.

Kiongozi wa walio wachache katika Bunge, Nancy Pelosi amesema: “Uongozi wa Trump tayari umeshakiuka kiapo cha uongozi kwani kile wanachokifanya sio tu kwamba ni kinyume cha katiba lakini kinawafanya wamarekani wasiwe salama.”

Waandamanaji wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa Dulles, Washington DC
Waandamanaji wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa Dulles, Washington DC

Maandamano yaenea nchi nzima

Wakati maandamano ya kupinga wahamiaji kuingia nchini yakienea nchi nzima, uongozi wa Trump umeendelea kudai kuwa rai ya jamii iko upande wao.
Msemaji wa White House Sean Spicer amesema:” Ni wazi kuwa wamarekani wengi wanaokadiriwa kupiga kura wanakubali kuwepo amri ya muda ya kukataza wakimbizi kutoka Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan, Yemen mpaka pale serikali itakapoweza kufanya kazi nzuri ya kuwazuia watu ambao ni tishio.”

Katika jamii zenye waislamu wengi nchini Marekani, kama huko Dearborn, Michigan amri inayopiga marufuku waislam imeleta wasiwasi mkubwa, amesema mwakilishi wa eneo hilo.

Wahamiaji wana wasiwasi mkubwa

Mwakilishi Debbie Dingell wa Demokratik amesema: "Inatosha peke yake kuona wasiwasi ulioko moyoni na rohoni mwao, kwamba kuna siku mtu atapiga hodi katika mlango wao saa tisa alfajiri na kuwachukua wakiwa bado wamelala vitandani mwao na kuwaondosha nchini,” Dingell amesema thamani itakayolipwa na utekelezaji wa amri hii ya kiutendaji itakuwa kubwa.

“Sisi kwa pamoja tunataka kulinda usalama wa taifa letu lakini ukweli wa mambo ni kuwa usalama wa taifa unamaanisha ni pamoja na kulinda nguzo muhimu za Katiba yetu ambayo ni uhuru wa kuabudu".
Wapinzani wanasema kuwa katazo hili linachafua taswira ya Marekani, na usalama, katika nchi hizo ambazo zinalengwa na katazo hili, na mwanadiplomasia mkongwe ana wasiwasi—inaweza kuathiri ulimwengu mzima wa kiislamu.

Rai ya Mwanadiplomasia

Mwanadiplomasia huyo mstaafu Thomas Countryman amesema: “ Marekani siku zote imekuwa ikiwakaribisha, nchi iliyo fungua milango yake kwa wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi zote duniani, na dini zote, kwa miaka mingi. Na matarajio yangu kuwa watatambua kuwa hii ni amri ya muda, lakini na wasiwasi kuwa namna ilivyotangazwa na namna ya utekelezaji wake itatoa tafsiri potofu.”

Spika haungi mkono lakini...

Paul Ryan
Paul Ryan

Lakini Spika wa Bunge, Paul Ryan amewaambia waandishi kuwa hawezi kuunga mkono amri hiyo ya kuwazuia waislamu lakini anaiona kama ni hatua ya kusitisha uhamiaji kwa sababu za msingi.

Spika huyo amesema: “ Baada ya shambulio la Paris, ilikuwa wazi kwetu kwamba mmoja wa magaidi alijiingiza katika mkusanyiko wa wakimbizi wa Syria, kwa hiyo tulikuwa tunataka kuhakikisha hilo halitokei hapa nchini, na hiyo ni usalama wa taifa 101.”

Hiyo ni dalili ya kutosha kwamba ingawa wapinzani wanapigana juu ya kuizuia amri hiyo mahakama, White House ya Trump haiwezi kusalimu amri.

XS
SM
MD
LG