Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 03:26

Uhalifu dhidi ya Waislam Marekani waongezeka- Tafiti


Waislam wakilaani vitendo vya ugaidi
Waislam wakilaani vitendo vya ugaidi

Uhalifu unaowalenga Waislam wa Marekani unaosababishwa na chuki umeongezeka kwa asilimia 15 mwaka 2017, ikiwa ni mara ya pili kuongezeka kwa hali hiyo, kwa mujibu wa tafiti iliotolewa Jumatatu na kikundi cha Waislam, Council on American-Islamic Relations (CAIR).

Kikundi hicho kimebaini uhalifu unaotokana na chuki ukiwalenga Waislam mwaka 2017, kati ya matukio hayo ikiwemo kupigwa kwa mwanamume wa Kiislam katika eneo la Bronx la mji wa New York kwa kushambuliwa na watu waliomwita gaidi.

Tukio jingine ni la mwezi Novemba ambapo mgahawa unaomilikiwa na familia ya Kiislam, Kansas ulichomwa moto. Hilo liliongeza matukio hayo kutoka 260 mwaka 2017.

Taasisi hiyo ya Kiislam CAIR imeeleza ongezeko kuwa linatokana na sera za Rais wa Marekani Donald Trump, na hasa katazo la wahamiaji kutoka nchi zilizo na Waislam walio wengi.

“Hakujawahi kuwepo kitu kama hivi abadan, kwa jumuiya ya Waislam kuwa ni wanyonge wa Rais wa Marekani ambaye amekuwa akiwashambulia,” amesema Gadeir Abbas, wakili wa CAIR.

Akijubu kwa njia ya barua pepe kuhusu maoni ya madai haya, msemaji wa White House Kelly Love amesema, “Utawala wa Trump unafuata sheria na unachukia aina zote za uvunjaji sheria ikiwemo uhalifu unaotokana na chuki.” Rais Trump ameendelea kulaani uvunjifu wa amani, ubaguzi na makundi yenye kutengeneza chuki.”

Wakati akiwa mgombea wa urais, Trump aliahidi “kusitisha kabisa kuingia Waislam nchini Marekani.” Mara baada ya kuingia madarakani alisaini amri ya kiutendaji ikipiga marufuku wasafiri kutoka nchi kadhaa zenye Waislam walio wengi kuingia Marekani.

Amri hiyo ambayo ilifanyiwa marekebisho, na kuiingiza Korea Kaskazini, ilianza kutumika mwisho wa mwaka 2017.

XS
SM
MD
LG