Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 11:32

Mahakama Ubelgiji yawahukumu wawili miaka 20 kwa jaribio la kigaidi


Salah Abdeslam na Sofien Ayari

Mahakama moja nchini Ubelgiji imewahukumu watu wawili kutumikia kifunguo cha miaka 20 waliokutikana na hatia ya jaribio la kigaidi la kumuuwa polisi kuhusiana na shambulizi la bunduki la mwezi Machi 2016 huko Brussels.

Wote wawili waliokutikana na makosa –Salah Abdeslam na Sofien Ayari- hawakuwako mahakamani Jumatatu wakati kesi hiyo inaamuliwa.

Abdeslam yuko jela nchini Ufaransa akisubiri kesi yake kusikilizwa juu ya kushiriki kwake katika shambulizi la kikundi cha Islamic State (IS) huko Paris Novemba 2015.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa peke yake ndiye aliyesalimika katika kikundi cha IS ambao walijitoa muhanga.

Juu ya kuwa watu hao wawili walikuwa hawajafika mahakamani, kulikuwa na ulinzi mkali katika eneo hilo la mahakamani nje na ndani ya mahakama.Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG