Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 20:37

Jaji Marekani aongeza muda zuio la katazo la Trump


Mahakama ya serikali kuu
Mahakama ya serikali kuu

Jaji wa Mahakama ya serikali kuu ameongeza muda wa kusimamisha kwa muda amri ya kiutendaji ya Rais Donald Trump inayopiga marufuku watu kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi na pia wakimbizi kuingia Markani.

Jaji huyo wa wilaya Derrick Watson alikuwa amezuia kwa muda, serikali kutekeleza agizo la kiutendaji Machi 15.

Uamuzi wake mpya Jumatano ulienda mbali zaidi, ukiweka katazo la awali (kabla kesi haijatolewa uamuzi) dhidi ya amri ya Trump, kwa ombi lilokuwa limeletwa na jimbo la Hawaii, ambalo linahusisha nchi nzima.

Watson ameandika mazingira yaliyopelekea kupitisha uamuzi wa mwanzo haujabadilika, Hawaii wakitoa hoja kuwa kauli ya Trump na washirika wake iliwalenga Waislamu peke yao.

Jaji huyo amesema jimbo limejiridhisha kuwa kuna uwezekano kuwa itashinda katika kulipinga katazo hilo kwa misingi ya kuwa inavunja vipengele vya katiba vinavyotaka hatua za serikali ziwe na lengo la misingi ya kisekula na sio udini.

Kutoka katazo la Waislamu kwenda uchunguzi wa kina

Kampeni ya Trump ya kugombea urais mara moja iliwahi kutoa kauli juu ya kukataza Waislamu wote kuingia Marekani, sera ambayo baadae ilibadilika na kusisitiza kuwepo “uchunguzi wa kina” juu ya watu wanaotoka nchi ambazo zinahusishwa na ugaidi.

Uongozi wa Trump umesisitiza kuwa amri ya kiutendaji sio ni kwa ajili ya katazo la Waislamu, na rais ametoa hoja kuwa amri ya kiutendaji ni muhimu kwa kulinda usalama wa taifa.

Imehusisha katazo la utoaji viza kwa watu wa Iran, Syria, Libya, Yemen, Somalia na Sudan kwa siku 90, na kusitisha programu ya kuwatafutia makazi wakimbizi kwa siku 120. Katika nyakati hizi, upitiaji wa utaratibu wa uchunguzi na jinsi ya kuimarisha usaili huo unatakiwa ufanyike.

Watson amesema katika amri yake kuwa serikali imetoa hoja kuwa mahakama zipuuzie maudhui yanayo fungamana na agizo hilo.

“Mahakama haiwezi kukaa pembeni, kufunga mapazia na kujifanya haijaona kile ilicho kiona,” Watson ameandika.

Serikali pia imetoa hoja kuwa katazo lolote la mahakama litumike kwa zuio la viza peke yake na lisitumike dhidi ya katazo la wakimbizi kuingia Marekani. Lakini jaji amesema, “Haiingii akilini kufanya hivyo.”

Rais aahidi kuzipinga changamoto hizo

Trump ameahidi kuendelea kupambana na changamoto za kisheria zinazo ikabili amri yake, na kukata rufaa Mahakama Kuu ikiwa kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Idara ya Mwanasheria Mkuu Hawaii imeeleza wanaimani kuwa mahakama za juu zitaendelea kuwaunga mkono juu ya msimamo wao.

“Wakati tunatambua kuwa rais anaweza kukata rufaa, tunaamini maamuzi ya busara ya mahakama yatasimama imara,” Idara hiyo imesema katika ujumbe wa Twitter.

Amri ya katazo la kusafiri pia inapingwa katika mahakama ya serikali kuu iliyofunguliwa na jimbo la Maryland.

Kesi hiyo imekomea kwenye kusitishwa viza kwa nchi sita, na jaji wa Mahakama ya Wilaya ametoa uamuzi wa katazo hilo hilo ikiitaka serikali isitekeleze uamuzi huo.

Lakini Idara ya Sheria imekata rufaa juu ya uamuzi huo kwa mahakama ya nne ya rufaa, ambayo imepanga kusikiliza hoja Mei 8.

Kikundi cha wanasheria wa serikali katika majimbo 12 wamefungua muhtsari wa kesi na mahakama hiyo ya rufaa wakiunga mkono amri ya kiutendaji ya Trump, kwa hoja ya kuwa haimaanishi ni katazo kwa Waislamu

Majimbo hayo ni Alabama, Arizona, Arkansas, Florida, Kansas, Louisiana, Montana, Oklahoma, South Carolina, South Dakota, Texas na West Virginia.

Rufaa ya kesi iliyofunguliwa na Hawaii itakwenda mahakama nyingine, ambayo ni mahakama ya 9 za Mahakama za Rufaa za Marekani.

XS
SM
MD
LG