Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:51

Marekani, Iran zatupiana vitisho baada ya jenerali Qassem Soleimani kuuawa


Wanajeshi wa Miamvuli wakipakia vifaa na kupanda ndege katika kituo cha kijeshi cha Fort Bragg, North Carolina Januari 4, 2020. Wizara ya Ulinzi inasema wanajeshi hao wanapelekwa kufuatia kuongezeka vitisho dhidi ya wafanyakazi wa Marekani na vifaa vyao.
Wanajeshi wa Miamvuli wakipakia vifaa na kupanda ndege katika kituo cha kijeshi cha Fort Bragg, North Carolina Januari 4, 2020. Wizara ya Ulinzi inasema wanajeshi hao wanapelekwa kufuatia kuongezeka vitisho dhidi ya wafanyakazi wa Marekani na vifaa vyao.

Viongozi wa Marekani na Iran wametupiana vitisho kufuatia kuuawa kwa jenerali wa ngazi ya juu wa Iran kufuatia shambulizi la angani lililofanywa na Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameahidi kulipiza kisasi kufuatia kuuliwa kwa Qassem Soleimani.

Rais wa Marekani Donald Trump Jumamosi alitishia kufanya mashambulizi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini Iran iwapo nchi hiyo itachukuwa hatua yoyote ya kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya Soleimani.

Trump alituma ujumbe wa Tweet kwamba tayari imekwisha viorodhesha vituo 52 ndani ya Iran ambavyo Marekani itavishambulia “kwa haraka na nguvu kubwa” iwapo Iran itamshambulia mfanyakazi yoyote wa Marekani au mali zake. Idadi hiyo ya 52 inawasilisha Wamarekani waliokuwa wametekwa miaka mingi huko nyuma.

“Hivi sivyo ambavyo Marekani inatakiwa kufanya na kuna uwezekano ikakiuka mikataba na desturi za kimataifa,” Larry Pfeiffer, mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa kiusalama, sera na ulinzi wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha George Mason ameiambia Sauti ya Amerika.

Pfeiffer, ambaye ni mkurugenzi wa zamani wa Chumba cha Matukio cha White House amesema vitisho vya Trump vinafanana na tamko linalotolewa na serikali ya kidikteta kama vile Korea Kaskazini.

“Wakati rais wa Marekani anaporuhusu vitendo kama hivyo, anatoa uhalali potofu kwa mahasimu wa Marekani kufanya vivyo hivyo,” Pfeiffer amesema.

Trump alizungumzia Ijumaa juu ya kitendo cha kumuua Soleimani kwa mara ya kwanza tangu maafisa wa wizara ya ulinzi ya Marekani kuthibitisha jenerali wa Iran alikuwa ameuawa katika shambulizi la angani lililofanywa na Marekani.

XS
SM
MD
LG