Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:13

Iran haina nia ya kuongeza mivutano na Marekani - Zarif


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema mapema leo kuwa Iran haitaki kuongeza mivutano.

Hata hivyo Iran imesisitiza kuwa kila nchi inastahili kufurahia uhuru wake kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Waziri huyo amesema hayo wakati wa ziara yake nchini Japan. Rais Donald Trump aliiondoa Marekani kwenye mkataba wa kimataifa wa nyuklia na Iran wa mwaka 2015 na badala yake akaliwekea taifa hilo vikwazo zaidi.

Trump Jumatatu amesema kuwa ana azma ya kukutana na Rais wa Iran muda utakaporuhusu ili kutafuta suluhisho kuhusiana na mkataba wa nyuklia.

Pia anadhamira ya kuhakikisha kuwa uchumi wa Iran unaimarika. Hata hivyo Trump amesema kuwa hana nia ya kuondoa vikwazo dhidi ya taifa hilo.

Rais wa Iran Hassan Rouhani kwa upande wake amesema kuwa Iran haiko tayari kufanya mashauriano na Marekani hadi pale vikwazo vitakapoondolewa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG