Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 21:51

Waandamanaji Iraq wawasha moto mbele ya Ubalozi wa Marekani


Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la mpiganaji wa kikosi kinachosaidiwa na Iran aliyeuawa na shambulizi la anga lililofanywa na Marekani, wakati wa maziko yake huko Najaf, Iraq, Disemba. 31, 2019.

Maafisa wa usalama kwenye ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, Jumatano wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji.

Waandamanaji hao wanaongozwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran na wamekusanyika kwa siku ya pili sasa.

Baadhi yao wamekesha nje ya jengo hilo baada ya kundi kubwa kukaidi amri ya kutokaribia na kuwasha moto karibu na jengo hilo jana Jumanne.

Rais wa Marekani Donald Trump jana Jumanne alisema kuwa Iran italaumiwa kutokana na uharibifu wowote utakaotokea kwenye ubalozi huo.

Kupitia ujumbe wa tweeter, Trump alisisitiza kuwa Iran italipa gharama kubwa iwapo uharibifu wowote utatokea. Hata hivyo wakati akizungumza na wanahabari.

Trump alisema kuwa haoni uwezekano wa Marekani kwenda vitani na Iran.

Naye Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amekemea vitendo vya Marekani ndani ya Iraq na Syria huku akimjibu Trump kupitia ujumbe wa tweet kwamba hakuna chochote anachoweza kufanya dhidi ya taifa lake.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG