Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 13:54

Shambulizi la vituo vya mafuta Saudi Arabia na wasiwasi wa mafuta kupanda bei duniani


Vituo vya mafuta vya kampuni ya Saudi Aramco's vilivyoko Buqyaq, Saudi Arabia, vilivyoshambuliwa siku ya Jumamosi.

Wachambuzi wameonya kuwa shambulizi lililofanywa na ndege zisizokuwa na rubani (droni) katika vituo viwili vya mitambo ya kusafisha mafuta, inaelekea kuwa umezidi kuharibu uwezekano wa suluhisho kati ya Tehran na Washington, na huenda ukasukuma bei ya mafuta kufikia dola za Marekani 100 kwa pipa moja la mafuta.

Rais Trump ameonya Jumapili kuwa Marekani iko tayari kujibu mashambulizi yaliyofanywa kwa kutumia droni katika mitambo ya kusafisha mafuta nchini Saudi Arabia, ikisema Washington inajua nani aliyefanya shambulizi hilo.

"Tuko tayari kujibu mashambulizi lakini itategemea na uthibitisho utakaopatikana, lakini pia tunasubiri kupata taarifa kutoka Saudi Arabia juu ya yule aliyehusika na shambulizi hilo na makubaliano gani tutajibu shambulizi hilo”

Iran imekanusha kuhusika na shambulizi hilo la kutumia droni ambalo limeathiri uzalishaji wa mafuta kwa asilimia 5.

Waasi wa kikundi cha Kihouthi nchini Yemen wanaosaidiwa na Tehran wamedai kuhusika na shambulizi hilo, na kusema droni 10 zilitumika kushambulia vituo vya mafuta vya Abqaiq na Khurais, na kusababisha moto mkubwa. Kwa wiki kadhaa Saudi Arabia itakabiliwa na uhapa wa uzalishaji mafuta ghafi na gesi, maafisa wa Saudi wamesema.


Maafisa wa Marekani walitoa picha za satellite na kueleza habari za kijasusi zinazothibitisha kuwa Iran ilihusika na shambulizi hilo. Maafisa wa Marekani wanasema muelekeo na uwezo wa shambulizi hilo unaweka ulakini juu ya Wahouthi kuhusika.

Jenerali Amir Ali Hajizadeh, kamanda wa kikosi cha anga cha majeshi ya mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran, amesema Jumapili vituo au manuari za Marekani ziko kilomita 2000 ambapo makombora ya Iran yanaweza kuvifikia.

Shambulizi hili limekuja wakati Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa anafikiria kuondoa vikwazo juu ya Iran ikiwa ni hatua ya kuwahamasisha viongozi wa Iran kuingia katika mazungumzo kufikia makubaliano yanayotarajiwa kuzuia Iran kurejea upya katika hatua yake ya kuzalisha nyuklia.

Hatua ya Rais Trump kumfukuza kazi mshauri wake wa uslama wa taifa John Bolton – ikiwa inatokana na tafukuri ya rais, kulingana na ripoti za vyombo vya habari – ilileta matumaini kuwa angalau kutakuwa na uwezekano wa kupunguza mvutano uliopo kati ya Washington na Tehran.

Magazeti ya Iran yalifurahia kuondoka kwa Bolton, ambaye wamemtaja kama “moja wa maafisa wenye msimamo dhidi ya Iran” ambaye yuko karibu na Rais wa Marekani.

Wachambuzi wanasema kuwa Marekani na Iran wako katika ncha ya mgogoro kamili tangu Rais Trump alipoiwekea vikwazo Tehran mwaka 2018, aliposusia mkataba wa kimataifa uliokusudia kudhibiti harakati za Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG