Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:52

Kuendelea kwa viongozi wa Iran kutumia mitandao ya kijamii yaibua mjadala Marekani


Kiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei (Kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje Foreign Mohammad Javad Zarif
Kiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei (Kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje Foreign Mohammad Javad Zarif

Kuendelea kwa maafisa wa ngazi ya juu wa Iran ambao wamewekewa vikwazo na uongozi wa Rais Trump katika miezi ya karibuni imeiweka serikali ya Marekani na watendaji wa mitando ya kijamii katika hali ngumu.

Kiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammad Javad Zarif wameendelea kuwa wanatuma ujumbe mara kwa mara katika mitandao ya kijamii ya Marekani tangu Wizara ya Fedha ya Marekani kuongeza majina yao katika orodha ya mataifa maalum na watu wanaowekewa vikwazo (SDN) iliyochapishwa miezi ya Juni na Julai 2019.

“Katika hali hii uongozi ambao unajaribu kuweka shinikizo kubwa dhidi ya utawala wa Iran, lakini hawana uwezo wa kuondoa ushiriki wa waziri wa mambo ya nje katika mitandao ya jamii inayotengenezwa Marekani,” amesema aliyekuwa afisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi cha Wizara ya Mambo ya Nje cha Marekani Jason Blazakis. Hivi sasa afisa huyo anaongoza kituo cha kupambana na ugaidi katika Chuo cha Middlebury kinachofanya tafiti za kimataifa kilichopo Monterey, California.

“Nafikiri wanakabiliwa na hali ngumu inapokuja kuwafanya Silicon Valley wafanye wanachokitaka,” ameongeza Blazakis wakati akihojiwa na Sauti ya Amerika (VOA).

Amri ya kiutendaji

Rais wa Marekani alitaja Sheria ya dharura ya kimataifa ya Nguvu za Kiuchumi (IEEPA) ya mwaka 1977 wakati alipokuwa akitangaza amri ya kiutendaji mwezi Juni 2019 inayokataza utoaji huduma kwa Khamenei na yeyote mwengine ambaye anaonekana akitenda kwa niaba ya kiongozi huyo wa juu wa Iran, na amri hiyo pia ilitumika dhidi ya Zarif.

Lakini sheria hiyo (IEEPA) pia inalinda haki za Wamarekani katika kubadilishana habari na watu wa mataifa ya kigeni waliowekewa vikwazo, ili muradi tu taarifa hizo zisihusishe“kuhamisha habari yenye umuhimu,” kwa mujibu wa Huduma za Tafiti za Bunge la Marekani. Marekebisho ya sheria ya IEEPA mwaka 1988 na 1994 zinasema kubadilisha taarifa kama hizo zinahusisha habari mbalimbali katika aina mbalimbali za vyombo vya habari.

Hakuna ruhusa kubadilishana habari na jumuiya za kigeni za kigaidi (FTO) zilizotajwa na serikali ya Marekani kwani haki ya kubadilishana taarifa haipo katika kifungu cha 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia.

Uongozi wa Trump ulitaja Askari wa Jeshi maalum wa Jeshi la Kiislam la Mapinduzi la Iran (IRGC) kuwa ni FTO mwezi April, na kufanya mtandao wa Instagram kuondosha akaunti ya jeshi kamanda wa jeshi hilo Qassem Soleimani siku ya pili yake.

Ni kinyume cha sheria kwa Wamarekani hali wakiwa wanajua kutoa msaada wa vifaa au rasilmali” kwa FTO. Uongozi wa Trump unasema msaada huo unajumuisha “aina yoyote … ya huduma, ikiwemo… vifaa vya mawasiliano.”

Katika tamko lake la Mwezi April kwa vyombo vya habari vya Marekani, Instagram ilisema “inaendesha shughuli zake chini ya sheria ya vikwazo vya marekani… (na) inafanya au wanafanya kazi na vyombo husika vya serikali kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu ya kisheria, ikiwemo yale yanayohusiana na kutoa huduma kwa taasisi zilizotajwa kuwa ni za kigaidi ikiwemo jeshi la Iran.” Lakini haikutaja akaunti mahsusi zilizofungiwa.

Instagram, kampuni tanzu ya Facebook, na Twitter zilikataa kutoa maoni juu ya kile watakachofanya dhidi ya akaunti ya Zarif ilipoulizwa na Sauti ya Marekani (VOA).

XS
SM
MD
LG