Wine alikuwa anazuiliwa nyumbani kwake tangu uchaguzi wa rais katikati ya mwezi na kumesababisha shinikizo la kimataifa aachiliwe, wakili wake alisema Jumatatu.
Wanajeshi wamemzuia nyota huyo wa muziki mwenye umri wa miaka 38 aliyeingia kwenye siasa kutoka nyumbani kwake katika kitongoji cha mji mkuu wa Kampala.
Wine amekuwa akizuiliwa tangu alipopiga kura katika uchaguzi wa Januari 14 ambapo alishiriki katika kinyang'anyiro hicho akishindana na Rais wa muda mrefu Yoweri Museveni.
Jaji aliamuru kwamba serikali na vyombo vyake vya usalama wanapaswa kuondoka mara moja kwenye eneo lake na haki yake ya uhuru wa kibinafsi inapaswa kurejeshwa mara moja, wakili George Musisi aliiambia Reuters.