Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:28

Chama cha NUP cha Uganda kinapinga matokeo ya urais nchini humo


Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni (L) na Robert Kyagulanyi aliyekuwa mgombea urais wa NUP, Januari 14, 2021
Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni (L) na Robert Kyagulanyi aliyekuwa mgombea urais wa NUP, Januari 14, 2021

Mathias Mpuuga wa NUP anasema "tunao ushahidi wa kujazwa kura katika masanduku ya kupigia kura, na aina nyingine za uovu kwenye uchaguzi na baada ya kuweka vitu vyote pamoja, tutachukua hatua zote ambazo sheria inaruhusu kupinga udanganyifu huu"

Chama cha kiongozi wa upinzani Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine kimesema Jumapili kwamba kitapinga kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais uliofanyika Januari 14.

Tunao ushahidi wa kujazwa kura katika masanduku ya kupigia kura, na aina nyingine za uovu kwenye uchaguzi na baada ya kuweka vitu vyote pamoja, tutachukua hatua zote ambazo sheria inaruhusu kupinga udanganyifu huu, Mathias Mpuuga wa chama cha National Unity Party-NUP aliwaambia waandishi wa habari Jumapili siku moja baada ya tume ya uchaguzi Uganda kumtangaza Rais Yoweri Museveni mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais 2021.

Yoweri Museveni (L) na Robert Kyabulanyi maarufu Bobi Wine
Yoweri Museveni (L) na Robert Kyabulanyi maarufu Bobi Wine

Tangu alipochukua udhibiti wa Uganda mwaka 1986 Museveni mwenye miaka 76 ametawala Uganda muda wote. Anapuuzia madai ya udanganyifu wa katika uchaguzi wa wiki iliyopita dhidi ya Wine, mwenye miaka 38, msanii wa muziki aliyeingia katika siasa na kushikilia kiti cha Ubunge.

Tangazo la Jumapili kutoka chama cha upinzani NUP limekuja wakati watu wawili walimethibitishwa kufariki katika maandamano, tangu matokeo ya uchaguzi, liliripoti shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG