Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:58

Maambukizi ya COVID Afrika yapungua kwa wiki 16 mfululizo- WHO


FILE PHOTO: Mkurugenzi mkuu wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti. ( May 23, 2018. )
FILE PHOTO: Mkurugenzi mkuu wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti. ( May 23, 2018. )

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema nchi za Afrika zinaendelea kuripoti idadi ndogo ya maambukizi ya virusi vya Corona, tangu kuanza kwa janga hilo.

Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Corona kila wiki imepungua kwa wiki 16 sasa, sawa na idadi ya vifo katika muda wa wiki nane zilizopita.

Wataalam hata hivyo wanaonya kwamba huenda maambukizi yakaongezeka wakati wa msimu wa baridi hasa kusini mwa Afrika.

Mkurugenzi mkuu wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti, amesema kwamba kuna hatari kubwa sana ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona na kwamba kuna haja kubwa ya kutekeleza masharti ya kukabiliana na maambukizi hayo.

XS
SM
MD
LG