Tedros ameongeza kwamba ni wakati kwa ulimwengu kutadhmini ulichojifunza kutokana na janga hilo. Tedros ameomba mataifa yote yanayotengeneza chanjo yashirikiane na Umoja wa Mataifa katika kuimarisha uzalishaji pamoja na taarifa za kiteknolojia.
Kiongozi huyo ameongeza kusema kwamba ingawa baadhi ya mataifa yameondoa kanuni zilizowekwa, janga hilo bado halijamalizika. Chuo kikuu cha John’s Hopkins kinachofuatilia janga hilo kote ulimwenguni kimesema Ijumaa kwamba kufikia sasa kuna zaidi ya kesi milioni 465 za maambukizi kote ulimwenguni ,pamoja na zaidi ya vifo milioni 6 tangu kuzuka kwa janga hilo mwishoni mwa 2019.