Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:11

Moderna inatafuta uidhinishwaji kwa watoto chini ya miaka 6


Chanjo ya Moderna ya COVID-19 inatafuta uidhinishwaji wa FDA kwa matumizi ya watoto walio chini ya miaka 6
Chanjo ya Moderna ya COVID-19 inatafuta uidhinishwaji wa FDA kwa matumizi ya watoto walio chini ya miaka 6

Chanjo ya Moderna ya COVID-19 inafanya kazi kwa watoto wachanga, wanaokua, na watoto wa chekechea, kampuni hiyo ilitangaza Jumatano maendeleo ambayo yanaweza kufungua njia kwa watoto wadogo kupata chanjo hiyo ikifika majira ya joto kama wasimamizi wakikubali.

Moderna ilisema katika wiki zijazo itawaomba wadhibiti nchini Marekani na Ulaya, kuidhinisha uchomaji wa dozi mbili ndogo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka sita. Kampuni hiyo inaangazia kuwa na dozi kubwa itakayoidhinishwa kwa watoto wenye umri wa kati na vijana nchini Marekani.

Tangazo hilo ni habari njema kwa wazazi ambao wamesubiri kwa shauku, ulinzi wa watoto wachanga na wamekuwa wakikatishwa tamaa mara kwa mara kwa vikwazo, na mkanganyiko kuhusu sindano zipi huwenda zikafanya kazi na ni lini. Watoto milioni 18 nchini Marekani walio chini ya umri wa miaka mitano, ndio kundi pekee la umri ambao bado hawajastahiki kupata chanjo.

Moderna inasema matokeo ya utafiti wa awali yanaonyesha watoto wanakua na viwango vya juu vya kingamwili za kupambana na virusi kutokana na sindano zinazokuwa na robo ya kipimo kinachotolewa kwa watu wazima.

Mara baada ya Moderna kuwasilisha takwimu zake kamili, idara inayosimamia ubora wa viwango vya chakula na dawa Marekani (FDA) italazimika kuamua kama alama hiyo muhimu inamaanisha kuwa vijana wanalindwa dhidi ya magonjwa mabaya kama watu wazima.

XS
SM
MD
LG