Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:17

Watu milioni 800 barani Afrika huenda waliambukizwa Covid 19 miaka miwili iliyopita-WHO.


 Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti, akishiriki mkutano kwenye makao makuu ya WHO mjini Geneva, Mei 23, 2018. Picha ya Reuters.
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti, akishiriki mkutano kwenye makao makuu ya WHO mjini Geneva, Mei 23, 2018. Picha ya Reuters.

Zaidi ya theluthi mbili za Waafrika wanaweza kuwa waliambukizwa virusi vya Covid katika miaka miwili iliyopita, ikiwa ni mara 97 zaidi kuliko idadi ya maambukizi iliyoripotiwa, ripoti ya shirika la afya duniani(WHO) imeeleza Alhamisi.

Vipimo vya kimaabara vimegundua visa milioni 11.5 vya Covid 19 na vifo 252,000 katika bara zima la Afrika kulingana na ripoti hiyo.

Kufikia mwezi Septemba mwaka jana, inawezekana kuwa watu milioni 800 walikuwa tayari wameambukizwa.

Lakini WHO kanda ya Afrika imesema utafiti wake ambao bado unakaguliwa unakadiria kwamba idadi rasmi ya maambukizi iliyothibitishwa huenda ikawa ndogo sana kuliko kiwango halisi cha maambukizi ya virusi vya corona barani Afrika.

“Ukaguzi mpya wa utafiti kwa kutumia vigezo sahihi umebaini kwamba idadi halisi ya maambukizi inaweza kuwa mara 97 zaidi ya idadi ya visa vilivyothibitishwa,” amesema mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti.

Ripoti hiyo ilikagua zaidi ya tafiti 150 zilizochapishwa kati ya Januari 2020 na Disemba mwaka jana.

“Kwa hali halisi, hii inamaanisha kuwa mwezi Septemba 2021, badala ya visa milioni 8.2 vilivyoripotiwa, kulikuwa na visa milioni 800,” amesema Moeti.

Kutokana na changamoto za kufika kwenye vituo vya upimaji kwa wananchi wa Afrika, maambukizi mengi hayakugunduliwa, kwa sababu upimaji ulifanywa kwa wagonjwa wanaolazwa hospitali ambao hawana dalili za ugonjwa wa Covid na wasafiri ambao walitakiwa kuonyesha matokeo ya vipimo vya haraka (PCR), yanayodhihirisha kwamba hawakuambukizwa.

XS
SM
MD
LG