Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 09:09

Amri kali zatekelezwa Shanghai kudhibithi Covid - 19


Mtu akinunua mafuta ya kupiga kupitia juu ya kizuizi katika soko lililowekewa amri ya watu kutotoka nje katika kupambana na virusi vya Corona, Shanghai, China. April 13 2022 PICHA: REUTERS
Mtu akinunua mafuta ya kupiga kupitia juu ya kizuizi katika soko lililowekewa amri ya watu kutotoka nje katika kupambana na virusi vya Corona, Shanghai, China. April 13 2022 PICHA: REUTERS

Baadhi ya wakaazi wa mji wa Shanghai, wameruhusiwa kuondoka majumbani mwao kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya wiki mbili, wakati mji huo ambao kwa kawaida una shughuli nyingi za kibiashara, unachukua hatua muhimu katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Maafisa wamesema kwamba karibu watu milioni 4.8 mjini Shanghai, wenye jumla ya wakaazi milioni 25, wamegundulika kuwa katika hatari ndogo sana ya kuambukizwa virusi vya Corona, katika muda wa wiki mbili.

Japo baadhi ya watu wameruhusiwa kuondoka majumbani mwao, hakuna taarifa za uhakika iwapo wanaruhusiwa kutembea bila vizuizi vyovyote, wengi wao wakisubiri kupata ruhusa kutoka kwa kamati maalum katika mitaa wanayoishi.

China imechukua hatua madhubuti za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona lakini bado kuna hatari kubwa ya maambukizi zaidi.

Naibu wa mkurugenzi wa tume ya afya ya kitaifa Lei Zhenglong, amesema kwamba zaidi ya watu 10,000 wameambukizwa Corona katika mda wa wiki moja, na kwamba maambukizi katika jamii hayajadhibitiwa kikamilifu.

Maambukizi ya virusi vya Corona nchini China ni ya chini sana ikilinganishwa na sehemu nyingine duniani, lakini serikali imeweka amri kali kuhakikisha kwamba maambukizi yanakoma kabisa.

XS
SM
MD
LG