Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 07:45

Mashirika 16 ya kiraia yaiomba IMF kutoa dola trilioni 2.5 kwa nchi maskini.


Nembo ya IMF ikionekana ndani ya makao make makuu mjini Washington baada ya mkutano wa kila mwaka wa IMF na Benki ya dunia. Oktoba 9, 2016. Picha ya Reuters.
Nembo ya IMF ikionekana ndani ya makao make makuu mjini Washington baada ya mkutano wa kila mwaka wa IMF na Benki ya dunia. Oktoba 9, 2016. Picha ya Reuters.

Mashirika 16 ya kiraia Jumanne yamelisihi shirika la kimataifa la fedha( IMF) kutoa dola trilioni 2.5 katika akiba yake ya dharura ili kuzisaidia nchi maskini ambazo bado zinashindwa kujikwamua kutokana na janga la Covid 19 na athari zake za kiuchumi.

Katika barua pepe kwa IMF na maafisa wa masuala ya kifedha kutoka kundi la G20 la nchi zilizoendelea kiuchumi, mashirika hayo ya kiraia yamesema nchi maskini tayari zilikuwa nyuma, na sasa masaibu yao yamechangiwa na kupanda kwa bei ya nishati na chakula vinavyochochewa na vita vya Ukraine.

Yamesema kitita cha dola bilioni 650 zilizotolewa mwaka jana na IMF, kiwango cha juu kuwahi kutolewa na taasisi hiyo ya kifedha, zilizisaidia nchi maskini kununua chanjo, kufufua uchumi wao na kuwekeza kwenye mifumo ya afya, lakini msaada zaidi bado unahitajika.

Nchi 99 zenye pato la chini na la kati zilitumia dola bilioni 104 kutoka kwenye akiba yao ya dharura tangu mwezi Agosti, lakini IMF ilitoa dola bilioni 400 kwa nchi zinazoendelea kiuchumi ambazo hazikuwa zinahitaji pesa hizo, mashirika hayo ya kiraia yamesema.

XS
SM
MD
LG