Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 03:22

Kesi ya BBI : Musyoka awataka Wakenya kuheshimu maamuzi ya mahakama


 Raila Odinga (Kushoto) na Kalonzo Musyoka.
Raila Odinga (Kushoto) na Kalonzo Musyoka.

Kiongozi wa chama cha Wiper nchini Kenya Kalonzo Musyoka ameungana na wanasiasa wengine wa zamani wa chama cha siasa cha NASA akitaka Wakenya kuheshimu maamuzi ya Mahakama ya Rufaa yaliyotolewa jana dhidi ya kesi ya BBI.

Katika taarifa yake aliyoitoa Ijumaa aliwataka Wakenya kuheshimu maamuzi hayo akisema kuwa hakuna taifa litakalo kua bila utawala wa sheria.

Kiongozi huyo wa Wiper pia amesema hakuna mtu aliyeanguka kupitia maamuzi hayo akigusia kwamba demokrasia yenye nguvu itaongoza Kenya. .

Hata hivyo Waziri Mkuu wa zamanni Raila Odinga kwa upande wake amesema wakati umefika wa kusonga mbele na kwamba pande zote zilizokuwa zinahusika katika utaratibu huo zitafanya maauzi yao binafsi ya jinsi ya kuendelea mbele.

Amesema uamuzi huo sio mwisho wa kuendelea na mazungumzo ya kutathmini katiba na kwamba juhudi za BBI hazikuwa mwisho wa safari.

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amesema umefika wakati wa kuzingatia mambo mengine muhimu kama vile kufufua uchumi na kudhibiti janga la COVID-19.

XS
SM
MD
LG