Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 02:04

Taliban waendelea kuimarisha utawala wao Afghanistan


Wapiganaji wa Taliban wakifanya doria katika mji mkuu wa Kabul, Aug. 19, 2021.
Wapiganaji wa Taliban wakifanya doria katika mji mkuu wa Kabul, Aug. 19, 2021.

Taliban wanaendelea kuimarisha utawala wao nchini Afghanistan wakati kukiwa na ripoti za ghasia dhidi ya waandamanaji katika jimbo la mashariki mwa nchi hiyo.

Taliban wanaendelea kuimarisha utawala wao nchini Afghanistan wakati kukiwa na ripoti za ghasia dhidi ya waandamanaji katika jimbo la mashariki mwa nchi hiyo, siku moja baada ya kundi la Kiislamu kutangaza vita vimekwisha na hakutakuwa na kulipiza kisasi kwa namna yoyote.

Mashuhuda wanasema waasi wa Taliban walifyetua risasi hewani na kuwapiga watu kwa virungu katika jiji la Jalalabad, ambapo kundi la waandamanaji walijaribu kushusha bendera ya Taliban na kupandisha bendera ya kitaifa ya Afghanistan Jumatano. Takriban watu watatu waliuawa na wengine wengi walijeruhiwa. Taliban hawakutoa maoni yao juu ya jambo hilo.

Mamia ya wanajeshi wa marekani wamewasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul kusaidia juhudi za kuwasafirisha maelfu ya wamarekani, raia wa Ulaya na wafghanistan wanaoendelea kuwasili kwenye uwanja huo.

Mwenyekiti wa majeshi ya Marekani Jenerali Mark Milley amehakikisha kwamba Wamarekani wote wataondolewa kutoka Afghanistan na wanashirikiana na viongozi wa Taliban kuwaondoa wamarekani.

XS
SM
MD
LG