Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:25

Waziri mkuu wa Sudan afanya ziara Sudan Kusini


Waziri mkuu wa Sudan Abdullah Hamdok ,kushoto, akiwa na waziri wa fedha wa Marekani mapema mwaka huu
Waziri mkuu wa Sudan Abdullah Hamdok ,kushoto, akiwa na waziri wa fedha wa Marekani mapema mwaka huu

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok Alhamisi amewasili Juba kwa ziara ya siku mbili kwa mazungumzo yenye lengo la kuboresha juhudi za amani nchini  Sudan Kusini, huku kukiwa na mzozo wa  kisiasa ambao ulimuondoa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, kama kiongozi wa upinzani. 

Maafisa kutoka Khartoum pamoja na wenzao wa Juba wanatarajiwa kuzungumzia uhusiano wa mataifa hayo mawili pamoja na utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Juba yaliyotiwa saini mwaka jana kati ya serikali ya Sudan na makundi kadhaa yenye silaha.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Mariam al Mahdi ambaye alifuatana na Hamdok amewaambia wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba muda mfupi baada ya kuwasili kuwa, kuna wasiwasi kwamba utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini unajikokota.

Hamdok amepangwa kukutana na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Machar, wanasiasa wengine wa ngazi ya juu, pamoja na wanadiplomasia kutoka Marekani, Uingereza na Norway.

XS
SM
MD
LG