Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:52

Wanawake kunufaika kwa dola bilioni 40


Mkuu wa shirika la wanawake la UN Women,Phumzile Mlambo-Ngcuka,
Mkuu wa shirika la wanawake la UN Women,Phumzile Mlambo-Ngcuka,

Mkuu wa shirika la wanawake la Umoja wa mataifa anayeondoka, Phumzile Mlambo Ngcuka ana matumaini  kuwa katika kipindi cha miaka 5, dola bilioni 40 zilizoahidiwa zitasaidia karibuni kuhamasisha usawa wa jinsia. 

Ngcuka amesema fedha hizo zitapelekea wanawake zaidi kuingia kwenye nyadhifa za uongozi, kupunguza manyanyaso dhidi ya wanawake, pamoja na kuinua hali ya kiuchumi ya zaidi ya wanawake milioni 40 waliyotumbukia kwenye umaskini kutokana na janga la corona.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Ngcuka amesema katika mahojiano kabla ya kujuzulu kama mkuu wa shirika la UN Women, baada ya kuhudumu kwa miaka 8. Ameongeza kusema kuwa anaamini wahisani kutoka sekta binafsi pamoja na mashirika, wata heshimu ahadi walizotoa wakati wa kongamano la kuzungumzia usawa la Generation Equality Forum, lililomalizika Julai 2 mjini Paris Ufaransa. Amesema kuwa kikao ni cha kihistoria katika kuangazia masuala tofauti yanayohusu wanawake.

XS
SM
MD
LG