Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 14:11

Kenyatta aongeza muda wa kutotoka nje usiku kwa siku 30


Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa amri ya kutotoka nje usiku na kupiga marufuku uuzaji wa pombe katika migahawa ikiwa ni sehemu ya juhudi ya kudhibiti maambukizi ya COVID-19.

Akilihutubia taifa Jumatano, Rais amesema amri hiyo ni ya nchi nzima kuanzia saa tatu usiku hadi za kumi alfajiri itaendelea kwa siku 30 zaidi, limeripoti gazety la The Nation la nchini Kenya.

Kenyatta pia ameongeza siku zaidi za kufungwa baa na vilabu vya pombe kwa siku 30 lakini ameruhusu mahoteli kuuza pombe kwa wageni wanaofikia katika hoteli hizo. Migahawa inatakiwa kufungwa saa mbili usiku, Rais amesema.

Idadi ya watu wanaohudhuria maziko na harusi imeongezwa kutoka watu 15 hadi 100 wakitakwa kufuata masharti ya afya, Kenyatta amesema.

Hotuba hiyo inafuatia mkutano wake rais na Kamati ya Taifa Inayokabiliana na Hali ya Dharura.

Hili limetokea wakati nchi ya Kenya ikiwa imeripoti maambukizi 213 mapya ya COVID-19 Jumanne, ikiongeza idadi ya maambukizi yaliothibitishwa kufikia 33,016 nchi nzima.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Afya, vifo vitano vipya vimefanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 564. Hivi sasa watu wasiopungua 19,296 wamepona kutokana na COVID-19.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG