Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 04:44

Jeshi Ufilipino laendelea kutafuta 'black box' ya ndege iliyoanguka


Waokoaji wakiutoa mwili wa aliyefariki katika ajali ya ndege ya kijeshi C-130 Hercules katika mji wa Patikul Mkoa wa Sulu, kusini mwa Ufilipino on Julai 4, 2021.
Waokoaji wakiutoa mwili wa aliyefariki katika ajali ya ndege ya kijeshi C-130 Hercules katika mji wa Patikul Mkoa wa Sulu, kusini mwa Ufilipino on Julai 4, 2021.

Maafisa wa usalama wa Ufilipino wanaendelea leo jumatatu kutafuta kwenye eneo la mashamba ya minazi boxi la kunasa mawasiliano ya ndege (black box) ya kijeshi iliyopata ajali Jumapili.

Boxi za kunasa mawasiliano ya usafiri wa ndege hurikodi yale yanayojiri wakati ndege ikiwa safarini na hutoa vielelezo kwa wachunguzi pale ndege inapopata ajali.

Ndege hiyo ya Kijeshi ilisababisha vifo vya watu 50, ikiwa moja wapo ya ajali mbaya kabisa ya ndege ya kijeshi kutokea nchini humo.

Wakati huohuo Maafisa wa jeshi wanasema wameshapata miili ya watu watano wa mwisho waliofariki kutokana na ajali ya ndege ya aina ya C130 Hercules.

Ndege hiyo ilishindwa kusimama kwenye njia ya ndege ilipokuwa inatua jana kwenye uwanja wa ndege wa Jolo katika jimbo la Sulu, ikiwa inawasafirisha wanajeshi 96.

Eneo ambapo ndege ya kijeshi ilipoanguka, katika mji wa Jolo, Ufilipino.
Eneo ambapo ndege ya kijeshi ilipoanguka, katika mji wa Jolo, Ufilipino.

Ndege iligonga minazi nje ya uwanja wa ndege na kulipuka kwa moto ajali iliyoshuhudiwa na wanajeshi na wakazi wa vijiji vya karibu.

Meja jenerali Edgard Arevalo aliwambia waandishi habari mjini Manila kwamba uchunguzi wa kina unafanyika kufahamu sababu za ajali hiyo.

Wamnajeshi polisi na wazima moto waliwaokoa wanajeshi 49 wakiwa ni pamoja na walioruka kutoka ndani ya ndege kabla ya ndege kulipuka na kuwaka moto.

Vyanzo vya Habari : AFP / AP

XS
SM
MD
LG