Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:23

Ajali ya ndege Ufilipino yaua 29 na kujeruhi 50


Mabaki ya ndege ya jeshi la Ufilipino C-130 Hercules. (Joint Task Force-Sulu via AP).
Mabaki ya ndege ya jeshi la Ufilipino C-130 Hercules. (Joint Task Force-Sulu via AP).

Watu wasiopungua 29 wamefariki na 50 kujeruhiwa Jumapili wakati ndege ya kijeshi ya Ufilipino ikiwa na wanajeshi ilianguka na kushika moto baada ya kutoka nje ya njia ya ndege kusini mwa nchi hiyo, maafisa wamesema.

Takriban watu 100, wengi wao wakiwa ni wahitimu wa jeshi, walikuwa katika ndege aina ya C-130 Hercules iliyokuwa inajaribu kutua katika kisiwa cha Jolo, kwenye jimbo la Sulu wakati wa mchana.

Baadhi ya wanajeshi walioonekana wakiruka kutoka katika ndege kabla ya kufika ardhini na kuwaka moto, amesema Meja Jenerali Williams Gonzales, kamanda wa kikosi kazi cha pamoja -Sulu.

Ilikuwa ni moja ya ajali mbaya sana za ndege ya jeshi nchini humo kuwahi kutokea.

“Hii ni siku ya kusikitisha, lakini ni lazima tuwe na matumaini,” Gonzales alisema katika taarifa yake.

“Tunaungana na taifa kuwaombea wale waliojeruhiwa na wale waliokufa katika ajali hiyo.”

Shughuli za uokoaji zinaendelea kwa watu 17 ambao hawajapatikana.

Chanzo cha Habari : AFP

XS
SM
MD
LG