Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:36

Jeshi la Msumbiji latangaza kuwaokoa raia zaidi ya 100


Watu waliolazimika kukimbia makazi yao huko Palma wakusanyika katika uwanja wa mpira wa Pemba kupokea misaada ya dharura huko Pemba Aprili 2, 2021.
Watu waliolazimika kukimbia makazi yao huko Palma wakusanyika katika uwanja wa mpira wa Pemba kupokea misaada ya dharura huko Pemba Aprili 2, 2021.

Jeshi la Msumbiji limesema zaidi ya raia 100 waliotekwa nyara na wanamgambo katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo la Cabo Delgado wameokolewa.

Kamanda wa jeshi Cristo-vao Chume amesema wengi wa waliookolewa ni wanawake na watoto, na kwamba wamekabidhiwa kwa serikali kwa usaidizi zaidi.

Kamanda huyo amesema wanamgambo wanaendelea kuwepo,katika wilaya ya Palma ingawa usalama wa eneo hilo unasemekana umedhibitiwa.

Jenerali huyo amesema wanamgambo wanaendelea kuteketeza nyumba katika baadhi ya vijiji.

Aliwashutumu wanamgambo hao kwa kutumia raia kama ngao jambo ambalo amesema linazifanya operesheni za kijeshi kuwa ngumu.

Serikali ilisema Jumanne vikosi vyake viliwaua zaidi ya waasi 150 katika wilaya ya Palma kati ya tarehe 21 na 23 Juni.

Katika siku za hifi karibuni jeshi la Msumbiji limeongeza juhudi zake katika vita dhidi ya wanamgambo katika jimbo hilo.

XS
SM
MD
LG