Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:07

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya  waridhia kupelekwa  ujumbe wa kijeshi nchini Msumbiji


Kambi ya wakimbizi huko Metuge ikiwa na wakimbizi waliokimbia mashambulizi ya wanmgambo kwenye mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Cabo Delgado.
Kambi ya wakimbizi huko Metuge ikiwa na wakimbizi waliokimbia mashambulizi ya wanmgambo kwenye mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Cabo Delgado.

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya Jumatano wameridhia kupelekwa ujumbe wa kijeshi nchini Msumbiji kusaidia kufundisha vikosi vyake vya kijeshi vinavyopambana na wanajihadi kaskazini mwa nchi, wanadiplomasia walisema.

Uasi mbaya wa wanamgambo wanaohusishwa na kundi la Islamic State umeuharibu mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Cabo Delgado tangu mwishoni mwa mwaka 2017, na kuua watu 3,000 na kusababisha wengine laki 8 kupoteza makazi yao.

Utawala wa zamani wa kikoloni, Ureno tayari unatoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji na wakufunzi wa jeshi la Lisbon walioko huko watakuwa sehemu ya ujumbe mpya wa Umoja wa Ulaya.

Mwanadiplomasia mwandamizi wa Ulaya alisema kuwa nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Italia, na Uhispania zinatarajiwa kutoa wafanyakazi katika ujumbe huo.

Wakufunzi wa jeshi la Lisbon walioko huko wataunda nusu ya ujumbe mpya wa Umoja wa Ulaya.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka kwa umoja wa mataifa 27 wanapaswa kusaini rasmi ujumbe huo kwenye mkutano wa Julai 12.

XS
SM
MD
LG