Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 13:21

Ajali ya ndege DRC yauwa watu 28


Ajali ya ndege iliyotokea Jumapili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ndege hiyo ilianguka katika eneo ya makazi ya watu huko Goma, Kivu Kaskazini Picha na Austere Malivika.

Watu ishirini na nane wamefariki huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kutokana na ajali ya ndege iliyokuwa imebeba watu 18 wakiwemo rubani wa 2 na abiria 16 na wengine 10 ni wakazi wa eneo ambapo ndege ilianguka.

Ndege hiyo ilianguka katika mji wa Goma, kwenye mtaa wa Birere wenye watu wengi karibu na mpaka wa Congo na Rwanda,

Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi ili kufahamu watu wangapi walikufa na wangapi walijeruhiwa.

Zoezi hilo linafanyika kwa msaada wa wananchi wa mji huo ambao waendelea kupekua nyumba za majirani zilizo angukiwa na ndege hiyo ya kampuni ya Beesyby.

Kampuni hiyo imekuwa ikifanya safari zake huko Kivu kaskazini ikisafiri kati ya miji ya Goma, Butembo na Beni.

Waziri wa Afia Kivu Kakule Kanyere Moise anasema kwa sasa ni mapema kusema watu wangapi waliofariki lakini mwandishi wetu Austere Malivika alishuhudia miili kumi na sita katika sehemu ya tukio na manusura mmoja.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Austere Malivika, DRC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG