Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 10:58

Ajali ya ndege Iran yaua watu 66


Ndege ya Iran Aseman Air
Ndege ya Iran Aseman Air

Ajali ya ndege ya abiria iliua watu 66 nchini Iran Jumapili, maafisa wa shirika la ndege nchini wamesema.

Kwa mujibu wa Shirika la mwezi mwekundu, kikosi chake cha uokoaji kilitumwa kwenda katika eneo lilioko karibu na mji wa Isfahan.

Ndege hiyo namba 3704 iliondoka Tehran kipindi cha usiku na kutoweka kutoka kwenye rada baadaye.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la Aseman, ilikuwa ikitokea mjini Tehran kwenda kusini magharibi wa mji wa Yasuf wakati ilipoanguka kwenye milima ya Zagros nchini humo.

Hata hivyo vyanzo vya habari nchini Iran vimesema kuwa hali ya hewa ndio iliyoletaN matatizo katika jitihada za uokoaji.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC ndege hiyo inaaminiwa kuwa ya miaka 20 iliopita na ilitengenezewa nchini Ufaransa.

Ripoti zinasema kuwa wale waliokuwa ndani ya ndege ni abiria 60, walinzi wawili, wahudumu wawili, rubani na msaidizi wake.

Miongo kadhaa ya vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran imeiacha nchi hiyo na ndege zilizotengenezwa miaka mingi iliyopita na ajali zimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG