Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 13:06

Ajali ya ndege Russia yaua watu 71


Mabaki ya ndege An-148 iliyopata ajali huko Russia

Abiria wote 71 waliokuwa ndani ya ndege ya abiria ya Russia waliuwawa wakati ndege hiyo ilipoanguka karibu na Moscow, maafisa wa Russia walisema Jumapili.

Ofisi ya uchunguzi wa safari huko Russia ilisema katika taarifa yake kwamba abiria 65 na wafanyakazi sita walikuwa ndani ya ndege na wote waliuwawa. Watoto watatu walikuwa miongoni mwa waathirika.

Ndege hiyo yenye miaka 7 ilipotea kutoka kwenye rada dakika kadhaa baada ya kuruka kutoka uwanjani kwa kasi ya mita 6,700 kwa saa katika sekunde za mwisho za ajali, kulingana na ripoti ya chombo kinachoangalia safari za ndege Flight Radar 24.

Ndege hiyo An-148 inayomilikiwa na shirika la ndege la Saratov ilisafiri kutoka Domodedovo kwenda mji wa Orsk wakati ilipopata ajali karibu na Argunovo kiasi cha kilomita 80 kusini-mashariki ya Moscow.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG