Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:27

Watu 15 wapoteza maisha katika ajali ya ndege Iran


Waokoaji wakiwa katika eneo la ajali na vyombo vya usalama vikifanya kazi pamoja baada ya ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 707 kuanguka uwanja wa ndege wa Fath magharibi mwa Tehran, Iran, Jumatatu, Jan. 14, 2019.

Ndege ya jeshi la Iran ya mizigo Boeing 707 ambayo ilikuwa imebeba nyama kutoka Kyrgyzstan imeanguka Jumatatu ilipokuwa inajaribu kutuwa magharibi mwa mji mkuu wa Iran, na watu 15 walio kuwa ndani yake wamepoteza maisha na mtu mmoja tu ndiye aliye salimika, vyombo vya serikali vimesema.

Shirika la habari la AP limeripoti kuwa ajali hiyo ya ndege imeshuhudia janga jingine la hivi karibuni la usafiri wa anga, ambapo ilikuwa na matumaini ya kubadilisha ndege zake kongwe kwa kununua mpya chini ya masharti ya makubaliano ya nyuklia ya 2015 baina yake na mataifa yenye nguvu duniani.

Lakini badala yake, kilicho tokea ni kujitoa kwa Rais Donald Trump kutoka katika makubaliano hayo mwezi May, ambapo kumezuia bilioni za dola katika mauzo yaliyo kuwa yamepangwa na kampuni ya Airbus na Boeing kuiuzia ndege Jamhuri ya Kiislam ya Iran, na hivyo kusitishwa huko kumeongeza hatari kwa abiria wanao safiri kwa ndege nchini Iran.

Ndege hiyo, ambayo ina fanya shughuli za kiraia, ilikuwa inajaribu kutuwa katika hali ya dharura majira ya saa mbili na nusu asubuhi, Jumatatu, katika uwanja wa ndege wa Fath, uwanja ambao uko chini ya mamlaka ya majeshi ya Revolutionary Guard. Ndege hiyo ilitoka nje ya njia yake wakati inatua, na kugonga uzio na kuingia katika makazi ya watu.

Televisheni ya serikali ya Iran ilionyesha picha za makazi hayo yaliyo chomeka na kuwa majivu na mabaki ya ndege yakiwa ardhini katika eneo karibu na makazi hayo. Moto mdogo ulikuwa unaendelea kuwaka pembeni ya ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa inatarajiwa kutuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Payam, karibu na ajali hiyo kiasi cha kilomita 40 (maili 25) magharibi mwa Tehran, mji mkuu wa Iran.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG