Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 17:32

Baraza la Usalama laijadili Iran


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) akutana na Rais wa Iran Hassan Rouhani (kushoto) pembeni ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa makao makuu ya UN, Septemba 25, 2018.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) akutana na Rais wa Iran Hassan Rouhani (kushoto) pembeni ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa makao makuu ya UN, Septemba 25, 2018.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) wa kila mwaka unaendelea Jumatano ambapo viongozi mbalimbali kutoka Iraq, Yemen, Afghanistan, Cuba na Uingereza watahutubia.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la UN linakutana pembeni kujadili, pamoja na mambo mengine, ushawisihi wa Iran katika Mashariki ya Kati na masuala yanayo husiana na udhibiti wa kuenea kwa silaha za maangamizi.

Mkutano huo utaongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amewataka viongozi wa dunia alipokuwa akihutubia mbele ya Baraza la Umoja wa Mataifa Jumanne “wautenge uongozi wa Iran muda wa kuwa wanaendelea na vitendo vya uchokozi."

“Uongozi huu hauheshimu majirani zake au mipaka yake au uhuru wa mataifa mengine. Badala yake, viongozi wa Iran wanaharibu rasilmali za taifa hilo kwa ajili ya kujinufaisha wao wenyewe na kueneza machafuko kila mahali Mashariki ya Kati na meneo mengine.," amesema Rais Trump Jumanne.

Trump amesisitiza kuwa makubaliano ya programu ya kutokomeza silaha za Nyuklia ya 2015, ambayo ameitoa Marekani katika mwafaka huo, ulikuwa “unawanufaisha viongozi wa Iran ”na kuisaidia bajeti ya jeshi lake kwa takriban asilimia 40 ambayo inatumika “kufadhili ugaidi na vurugu na mauaji huko Syria na Yemen.”

Rais amesema uongozi wake ulianza mwezi uliopita “ kurejesha vikwazo vikali dhidi ya programu ya nyuklia ya Iran ambavyo vilikuwa vimeondolewa katika makubaliano yaliyofikiwa na Iran” na vikwazo zaidi vitawekwa Novemba 5 na kuendelea.

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameliambia Baraza hilo katika hotuba yake kuwa hakuna nchi ambayo inaweza kulazimishwa kuja katika mazungumzo.

Rouhani amehoji vipi Iran inaweza kuingia katika mkataba na Marekani, ambayo amesema imekuwa ikienda kinyume na sera za kiongozi aliyemuachia Trump madaraka, Barack Obama.

Pia Rouhani ameutuhumu uongozi wa Trump kwa kujaribu kuzifanya taasisi zote za dunia kuwa ni dhaifu.

Katika mwaka alipozungumza kwa mara ya kwanza UN, Trump kuanzia hapo amepunguza ufadhili katika taasisi hiyo ya kimataifa, amejiondosha kutoka katika Makubaliano ya Tabia nchi ya Paris na mkataba wa nyuklia wa Iran, na kujitoa kutoka katika mashirika ya UN, likiwemo Baraza la Haki za Binadamu. Pia amekuwa na matatizo katika mikusanyiko ya viongozi wa G7 na Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO).

XS
SM
MD
LG